ASKARI 96 WA TANAPA WAMALIZA MAFUNZO YA AWALI WAAHIDI KUPAMBANA NA MAJANGIRI‏‎

Mkurugenzi mkuu wa TANAPA Allan kijazi akiwahutubia wahitimu wa mafunzo ya kuhifadhi maliasili katika chuo cha wanyama pori cha Mlele mkoani katavi ambao hawapo pichani hapo juzi katika chuo cha wanyama pori cha mlele ambapo wahitimu 96 walihitimu mafunzo ya awali ya wahifadhi wa rasilimali za nchi na aliwataka wafanye kazi kwa uadilifu mkubwa ili waweze kupambana na kutokomeza ujangiri na kuvunja mitandao ya majangiri ya ndani ya nchi na nje ya nchi.
 Askari wa hifadhi ya  mbuga ya wanyama (TANAPA)  wakiwa wamesimama wakimsikiliza mkurugenzi mkuu wa TANAPA  ambaye hayuko pichani wakati akifunga mafunzo ya askari hao waliohitimu mafunzo ya miezi 3 katika chuo wanyama pori cha Mlele mkoa wa katavi namna ya kulinda rasilimali za nchi ambapo amewataka wahitimu hao wafanye kazi kwa uaminifu
 
 Askari wa hifadhi ya  mbuga ya wanyama (TANAPA) wakiwa wamekaa wakimsikiliza mkurugenzi mkuu wa TANAPA ALLAN KIJAZI ambaye hayuko pichani wakati akifunga mafunzo ya askari hao waliohitimu mafunzo ya miezi 3 katika chuo wanyama pori cha Mlele mkoa wa katavi namna ya kulinda rasilimali za nchi ambapo amewataka wahitimu hao wafanye kazi kwa uaminifu.
 
*********************

HABARI KAMILI

Jumla ya askari 96 wa  Shirika  la Hifadhi la Taifa  la Wanyama Pori  (TANAPA) wametimu    mafunzo ya miezi   mitatu  katika
chuo     kipya   cha wanyama pori   cha Mlele  kilichopo Mkoa  wa Katavi  na kutoa kiapo cha uti  mbele ya Mkurugenzi
mkuu  wa TANAPA Allan Kijazi.
 
Askari hao  wa TANAPA walimaliza  mafunzo hayo  hapo juzi  kwenye chuo hicho   cha  wanyama Pori
cha Mlele  akiwa ni  mafunzo ya kwanza  hapa  nchini
kwa TANAPA  kutoa  mafunzo kama hayo kwa Askari wa wanyama pori kupatiwa mafunzo hayo  kabla ya kuanza  kazi.
 
Katika  Risala yao ya
wahitimu wa mafunzo hayo  ya
kulinda maliasili  iliyosomwa  na Bruno
Mbunda  walieleza kuwa
wamejifundisha  mbinu mbalimbali za
kulinda   rasilimali za Taifa  kwa Vitendo
na nadharia.
 
Waliyataja baadhi ya mafunzo waliyoyapata kuwa ni namna ya kufanya doria , kukamata  waharifu kumpekua  mharifu  na kutotumia nguvu  sana  katika kukamata  mharifu pamoja  na  pia wamejifundisha namna ya kutumia silaha
Walieleza  katika kipindi hicho cha  mafunzo
wahitimi   hao walifanikiwa kukamata  waharifu
hamsini  wakati  wakifanya
doria  katika maeneo mbambali ya
Mbuga ya  Katavi  na kwenye mapori ya akiba ya Rukwa  Lwafi
Wahitimu hao
walieleza kuwa  mafunzo hayo
yaliwashirikisha  Askari  99
lakini  watatu kati yao
wameshindwa  kuhitimu  zikiwemo
sababu  mbambali  kama
utoro na utovu  wa nidhamu   hari ambayo ilfanya wahitimu  waliomaliza kubaki  96 ambapo kati yao mwanamke  ni mmoja
na wanaume ni  95
Kwa upande wake
mkuu wamapori ya akiba  ya  Rukwa Lwafi
Joseph Mbung’ombe alimweleza mkurugenzi mkuu wa TANAPA kuwa chuo hicho
kinakabiliwa na changamoto mbalimbali
Alizitaja
changamoto hizo kuwa ni ukosefu wa mawasiliano
na  ubovu wa miundo  mbinu ya barabaa  na
upungufu  wa  magari pamoja
idadi ndogo ya washiriki  wa
mafunzo kwa wanawake na ufinyu  wa bajeti
Nae  Mkurugenzi  wa Hifadhi
na Ikolojia  Martini  Loibook  alieleza kuwa mafunzo hayo walioyapata
yanaumuhimu  sana  hasa kutokana na changamoto  zinazoikabili nchi  yetu
inayokabiliwa na wimbi la ujangili
Pia Mkurugenzi
wa  utumishi   na utawalla
wa TANAPA  Witnes Shoo  aliwataka wahitimu hao  kufanya kazi
kwa uaminifu  kwa kujituma  na
wawe na didamu  na  wasiwe na tabia ya kutow a siri za ofisi
Mkurugenzi
Mkuu   wa TANAPA  Allan Kijazi
aliwaasa wahitimu hao  wahakikishe
wanafanya kazi  zao kwa uaminifu
mkubwa  hasa  katika shughuli zao  katika kupambana kukomesha ujangili
Aliwataka
kutojihusisha  na masuala ya ujangiri na
badal awahakikishe wanafanya kazi za kupambana na mitandao ya ujangiri iliyopo
ndani ya nchi na nje ya nchi
Alisema wapo
baadhi ya watumishi wa TANAPA ambao wamekuwa sio waaminifu hivyo wahitimu hao
wahakikishe wanafanya kazi zao kwa uaminifu pasipo kueubuniwa na mtu yoyote
yule au watu

No comments

Theme images by sbayram. Powered by Blogger.