TANGAZO KUTOKA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA (NECTA)

Baraza
la Mitihani la Tanzania linapenda kuwakumbusha watu wote wanaotaka
kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) mwezi
Novemba, 2014 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba kipindi cha usajili
kilichoanza rasmi tarehe 1 Januari, 2014 kwa ada ya Shilingi
50,000/=kwa wanaojisajili CSEE na Shilingi 30,000/= kwa wanaojisajili
QT kitaishia tarehe 28 Februari, 2014.
Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz.
Kabla ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye
vituo vya mitihani kuchukua namba rejea (reference number) zinazotolewa
bure na kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au Mpesa.
Imetolewa na:
KAIMU KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA.
Leave a Comment