WARSHA YA MAFUNZO YA MFUMO WA BIASHARA YA HEWA UKAA YAFANYIKA BAGAMOYO
Washirki wa warsha ya mafunzo ya mfumo wa Biashara ya hewa ukaa mjini Bagamoyo Leo (Picha na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais)
……………………………………………………….
EVELYN MKOKOI
AFISA HABARI
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Kuongezeka
kwa kina cha bahari, kuongezeka kwa gesi joto, kupungua kwa barafu
hususan katika mlima Kilimanjaro na mabadiliko ya mfumo wa mvua,
Imeelezwa kuwa ni changamoto kubwa zitokanazo na athari za mabadiliko ya
tabia nchi nchini.
Hayo
yameelezwa leo na Mkurugenzi msaidizi kutoka Ofisi ya Makamo wa Rais
Mazingira, Bw Richard Muyungi katika ufunguzi wa warsha ya mafunzo wa
biashara ya hewa ukaa, mjini Bagamoyo iliyohusisha wataalam wa masuala
ya mazingira kutoka katika sekta mtambuka nchini.
Bw.
Muyungi ameeleza kuwa, Shughuli za kibinadamu hasa katika nchi
zilizoendela kama vile za uzalishaji viwandani zimekuwa zikichangia kwa
kiasi kikubwa katika kuleta athari za mabadiliko ya tabia nchi..na hii
inatokana na kuachiwa kwa kiasi kikubwa cha hewa ya ukaa kutoka
viwandani kwenda angani, ambapo ongezeko la joto ni kichocheo kikubwa
cha athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
Bw.
Muyungi aliongeza kuwa uzalishaji wa gasijoto katika maeneo mengine,
kama misitu, kilimo, joto, usafirishaji, majengo na methane huzalishwa
kwa kiasi kikubwa katika nchi zilizoendelea na uleta athari za
mabadiliko ya tabia nchi.
”Katika
nchi zinazoendelea umaskini ndo unasababisha ukataji ovyo wa misitu na
kuiuza kwa bei rahisi, aidha matumizi mabaya ya mbolea katika sekta ya
kilimo huchangia pia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa gesi joto.”
Alisisitiza
Tanzania
ni nchi mojawapo iliyoridhia mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya
tabia nchi tangu mwaka 1996 na itifaki ya Kyoto ya mwaka 2002 ukiwa na
lengo kubwa la kupunguza uzalishaji wa gesijoto.
Leave a Comment