JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu: 255 22 2460735/2460706-8
Faksi: 255 22 2460735/2460700
P.O. BOX 3056
DAR ES SALAAM
Barua pepe: met@meteo.go.tz
Tovuti: www.meteo.go.tz
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb Na: TMA/3000/5/Vol II 17 Machi, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA WADAU WOTE
Yah: Maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani
Tarehe 23 Machi, 2014
Kila
mwaka tarehe 23 Machi nchi wanachama wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani
hujiunga na kuadhimisha kuzaliwa kwa Shirika hilo lililoanzishwa tarehe
23 Machi, 1950 kulingana na kauli mbiu. Kauli mbiu ya mwaka huu ni ’Ushirikishwaji wa Vijana katika Masuala ya Hali ya Hewa’- ”(Weather and Climate: Engaging Youth)”.
Katika
kuadhimisha Siku ya Hali ya Hewa Duniani (WMO), Shirika la Hali ya Hewa
linawahamasisha vijana ulimwenguni kote kujihusisha na masuala ya hali
ya hewa, ili kupata maarifa na uelewa wa hatua za kuchukua katika
kipindi hiki cha mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Hatua hii ya WMO ni
muhimu kwa ustawi wa kizazi hiki na kijacho ili kujenga jamii imara
hapo baadae.
Siku
ya Hali ya Hewa Duniani ni siku ya kutafakari Juhudi zinazofanywa na
Wanasayansi Duniani katika kufahamisha Dunia kuchukua tahadhari juu ya
mabadiliko ya hali ya hewa duniani na athari zake. Mamlaka ya Hali ya
Hewa Tanzania inatoa wito kwa vijana wote kubadilika na kuchukua hatua
za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa katika kizazi hiki na
kuchukua tahadhari ili kizazi kinachokuja waweze kufaidi dunia yenye
mazingira bora zaidi. Vijana wote walioko mashuleni vyuoni na
wajasiriamali washiriki katika kuokoa dunia kutoka kwenye majanga
yaletwayo na mabadiliko ya hali ya hewa. Aidha chachu kubwa ni
kuhakikisha vijana wanakuwa mstari wa mbele katika kufuatilia taarifa za
hali ya hewa zitolewazo na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini.
Kama
ilivyo kwa wanachama wengine, Tanzania inaungana nao kuadhimisha siku
hii inayofikia kilele tarehe 23 Machi, 2014 kwa kuwakaribisha wananchi
wote kutembelea vituo vya hali ya hewa nchini ili kuona shughuli
zitolewazo na Mamlaka kuanzia tarehe 21-23 Machi 2014. Aidha, Mamlaka
itambelea na kutoa elimu kwa vijana wa baadhi ya shule na vyuo mbali
mbali kupitia ofisi zake zilizopo nchini kuanzia tarehe 19-20 Machi
2014. Kutoa statements/makala za siku hiyo kwenye magazeti, vipindi kwenye radio, na televisheni kuhusu ushirikishwaji wa vijana katika masuala ya hali ya hewa.
Mamlaka inawatakia maadhimisho mema ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani
’Ushirikishwaji wa Vijana katika Masuala ya Hali ya Hewa’
(Weather and Climate: Engaging Youth)
IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Leave a Comment