AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 13.05.2014.
- MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA KUKUTWA NA BHANGI.
TUKIO LA KWANZA.
MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI.
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA KITWANA S/O LUGOYA [30] MKAZI WA ILEMI-JUHUDI ALIUAWA KWA
KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA
KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI MAWE, FIMBO NA
MARUNGU. CHANZO NI TUHUMA ZA UNYANG’ANYI/KUTEKA GARI. AWALI TAREHE
12.05.2014 MAJIRA YA SAA 02:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MSHANGAMWELU,
KATA YA MSHEWE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE WILAYA YA MBEYA VIJIJINI
MKOA WA MBEYA. STEPHEN S/O MGOGO [40] MKAZI WA KABALE AKIWA NA WENZAKE
KWENYE GARI AINA YA FUSO WALIKUTA MAWE YAMEPANGWA BARABARA YA
MBALIZI/MKWAJUNI NA DEREVA ALIPOSHUKA ILI KUTOA MAWE HAYO LILITOKEA
KUNDI LA WATU WANNE KUTOKA VICHAKANI WAKIWA NA SILAHA ZA JADI MAPANGA
NA MARUNGU WALIWAVAMIA NA KUWASHAMBULIA KISHA KUWAPORA PESA, SIMU ZA
MKONONI NA PIKIPIKI MOJA T.682 CHT AINA YA SANYA ILIYOKUWA NDANI YA
GARI HILO NA KUTOWEKA KUSIKOJULIKANA. THAMANI HALISI YA MALI
ILIYOPORWA BADO KUJULIKANA. KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA PIKIPIKI
IMEPATIKANA NA WATUHUMIWA WAWILI 1. NDAYOBI S/O LUTEGO [26] MKAZI WA
IGUNGA-TABORA NA 2. IDDI S/O SADICK [29] MKAZI WA VETA WAMEKAMATWA.
MHANGA STEPHEN S/O MGOGO AMELAZWA HOSPITALI TEULE YA IFISI HALI YAKE
INAENDELEA VIZURI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI PINDI WANAPOWAKAMATA
WATUHUMIWA KWA TUHUMA MBALIMBALI BADALA YAKE WAHAKIKISHE WANAWAFIKISHA
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ICHUKULIWE. AIDHA
ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA
ALIYEKIMBIA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAKE. PIA KAMADA MSANGI ANATOA RAI KWA JAMII HUSUSANI
WAKULIMA NA WAFANYABIASHARA WA MAZAO KUEPUKA TABIA YA KUTEMBEA/KUWEKA
NDANI YA NYUMBA KIASI KIKUBWA CHA FEDHA ILI KUEPUKA MATATIZO
YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA MSAKO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI KATIKA
TUKIO HILO JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA NAYORAMU S/O WAJEKAJE [42]
MKAZI WA KIJIJI CHA MKWANGU NA MAJIGITA S/O MUSSA [40] MKAZI WA UVINZA
MKOANI KIGOMA BAADA YA KUKAMATWA WAKIWA NA NYARA ZA SERIKALI NYAMA
YA MNYAMA INSHA YENYE UZITO WA KILO 3 PAMOJA NA NGOZI YA KICHWANI YA
MNYAMA HUYO.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA TAREHE
12.05.2014 MAJIRA YA SAA 15:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
KISUNGU-MKWANGU, KATA YA MAMBA,TARAFA YA KIWANJA WATUHUMIWA NI
MTUMIAJI NI WAWINDAJI HARAMU NA TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI
KUFIKISHWA MAHAKAMANI.
KATIKA TUKIO LA PILI JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA
NAYORAMU S/O WAJEKAJE [42] MKAZI
WA KIJIJI CHA MKWANGU WILAYA YA CHUNYA BAADA YA KUKAMATWA AKIWA NA
BHANGI YENYE UZITO WA GRAMU 500.
MTUHUMIWA HUYO ALIKAMATWA TAREHE
12.05.2014 MAJIRA YA SAA 16:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MKWANGU,
KATA YA MAMBA,TARAFA YA KIWANJA WILAYA YA CHUNYA. MTUHUMIWA NI
MTUMIAJI NA MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI
KUMFIKISHA MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA
UWINDAJI HARAMU KWANI NI KINYUME CHA SHERIA, BADALA YAKE WAFUATE
TARATIBU ZILIZOPO KWA MUJIBU WA SHERIA ZA NCHI.
Imetolelewa na:
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Leave a Comment