ALGERIA YANUSA 16 BORA KOMBE LA DUNIA, YAITANDIKA KOREA KUSINI 4-2
TIMU ya Taifa ya Algeria imejiweka
mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya 16 ya kombe la dunia baada ya
kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-2 dhidi ya Korea kusini usiku huu.
Huu ni ushindi mzuri kwa Algeria hasa
baada ya Urusi kufingwa bao 1-0 na Ubelgiji, hivyo wawakilishi hawa wa
Afrika watahitaji pointi moja tu dhidi ya timu ya Urusi chini ya kocha
Fabop Capello.
Mabao Algeria yamefungwa na Slimani katika dakika ya 26, Halliche 28, Djabou 38, Yacine Brahimi 62.
Mabao ya Korea kusini yamefungwa na Son katika dakika ya 50 na Koo dakika ya 72.
Kikosi cha Algeria: Mbolhi, Bouguerra (Belkalem 89), Halliche, Mesbah, Feghouli, Brahimi (Lacen 77), Medjani, Slimani, Bentaleb, Djabou (Ghilas 73), Mandi Goals: Slimani 26, Halliche 28, Djabou 38, Brahimi 62
Leave a Comment