LUIS SUAREZ: NILIOTA WAKATI HUU KUFIKA KUTOKANA NA UKOSOAJI NILIOPATA KWA WAINGEREZA

Jembe la kazi: Luis Suarez alikuwa nyota wa Mchezo Italia ikiifunga England mjini Sao Paulo.
HABARI KAMILI
LUIS Suarez amekiri kuwa magoli yake
mawili ambayo yamewaacha England njia panda katika fainali za kombe la
dunia ni kisasi kitamu kutokana na ukosoaji waliofanya juu yake wakati
anacheza ligi kuu ya nchi hiyo.
Nyota huyo wa Uruguay na Liverpool
alifungiwa kwa kumfanyia ubaguzi wa rangi beki wa kushoto wa Ufaransa na
Manchester United, Patrice Evra. Pia kitendo chake cha kumung`ata kwa
meno beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic kilimufanya afungiwe katika
msimu wa utata kwake nchini England.
Baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya
England, Suarez, ambaye alicheza mechi yake ya kwanza tangu afanyiwe
upasuaji wa goti alisema: "Niliota jambo hili, Nafurahia muda huu,
kwasababu ya yote niliyoumia, ukosoaji niliopokea. Kwahiyo, mnaondoko."

Suarez, ambaye alikosa mechi ya ufunguzi ya Uruguay akishangilia bao la kwanza Sao Paulo

Shangwe: Akishangilia baada ya kufunga bao la pili Sao Paulo.
Suarez aliongeza: 'Kabla ya mchezo
watu wengi nchini England walicheka matatizo yangu miaka michache
iliyopita. Huu ni muda mzuri kwangu. Nataka kujua sasa wanawaza nini".
"Ulikuwa mchezo mzuri niliowahi kucheza. Ni muda wa ajabu kwangu. Labda siku mbili zilizopita sikuwaza kama ingewezekana".
Suarez alifunga bao la ushindi dakika tano kabla ya mpira kumalizika baada ya Wayne Rooney kusawazisha bao la kwanza.
Leave a Comment