Maalim Seif Afungua Mafunzo ya Majaji, Mahakimu,Wanasheria na Mawakili Zanzibar.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,
amevikumbusha vyombo vya sheria juu ya wajibu wa kushirikiana na
wananchi katika utekelezaji wa sheria, ili kuhakikisha kuwa haki
inatendeka kwa watu wanaokabiliwa na kesi mahamani.
Mhe.
Maalim Seif ametoa kauli hiyo katika hoteli ya Zanzibar Ocean View,
wakati akifungua mafunzo ya siku nne kwa majaji, mahakimu, wanasheria,
mawakili pamoja na kada nyengine za sheria.
Amesema
mara nyingi wananchi wamekuwa wakikosa haki zao mahakamani kwa madai ya
kuwepo sababu mbali mbali zikiwemo uchelewaji wa kesi, kukosekana kwa
mashahidi na mahakimu wa kundesha kesi hizo, na kutaka kuzingatiwa kwa
mambo hayo ili kuondosha vikwazo vya kupatikana kwa haki miongoni mwa
wananchi.
Amesema
katika kufanikisha masuala hayo, ni lazima vyombo vinavyohusika
kushirikiana kwa pamoja, ili kuona kuwa wananchi wanapata haki zao
zinazostahiki kwa wakati muafaka.
Makamu
wa Kwanza wa Rais, pia amesisitiza juu ya haki ya dhamana kwa
washitakiwa wanaoweza kupewa dhamana kwa mujibu wa sheria, na kwamba
kitu cha msingi ni kuwajengea mazingira bora washitakiwa hao ili waweze
kufika mahakamani pale wanapohitajika.
Aidha
amesisitiza haja ya kuzitazama sheria ambazo hazileti usawa na zenye
ubaguzi ndani yake, ili ziweze kubadilishwa na wananchi washirikishwe
katika mageuzi hayo.
Mapema
akizungumza katika mafuzo hayo, Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar
Mhe. Aboubakar Khamis Bakari amesema suala la uchelewashaji wa kesi
halizihusu mahakama peke yake, bali kuna wadau wengi wakiwemo mashahidi
na polisi ambao wanapaswa kushirikiana kikamilifu kuhakikisha kuwa
tatizo hilo linaondoka.
Leave a Comment