Moto mkubwa wateketeza soko la mitumba la karume jijini Dar es Salaam
Moto mkubwa umetetekeza kabisa soko kubwa la mitumba la karume jijini Dar es Salaam usiku wa Jumatano, na kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara wote wa soko hilo.
Wazima moto walifanikiwa
kuudhibiti moto uloweza kufikia karibu na kiwanda cha Breweries, lakini
haujasababisha hasara yeyote katika nyumba za jiranio wa soko hilo
kufuatana na mwandishi habari wa Raia Mwema Mbaraka Islam alipozungumza
na Sauti ya Amerika.
Anasema hakuna kibada cha
biashara kilichosalimika na hakuna mtu aliyefanikiwa kuokowa mali yake.
Mfanya biashara Wilson magembe anasema amepoteza kila kitu na ilikuwa
vigumu kuweza kuchukua bidhaa zao kwa sababu moto uliwaka kwa haraka
sana. ( PICHA KWA HISANI YA JAMII FORUM)

Leave a Comment