WACHEZAJI WA CAMEROON NA CROATIA WABADILISHA 'VICHUPI' BAADA YA MECHI
NYOTA
wa Croatia, Ivan Rakitic na Stephane M’Bia wa cameroon jana
walibadilishana bukta baada ya mechi ya Kundi A Kombe la Dunia baina
ya time hizo.
Licha
ya Rakitic kuiongoza Croatia kuifumua timu ya M'Bia mabao 4-0 na
kuwatupa nje ya michuano, wachezaji hao wawili wa zamani wa Sevilla bado
walitaniana na kubadilisha vifaa vya mchezo.
Wachezaji
wote walikuwamo kwenye kikosi cha Sevilla kilichotwaa taji la Europa
League msimu uliopita, lakini Unai Emery amewapoteza wote Rakitic
akisaini Barcelona na M'bia akirejea klabu yake mama, QPR.

Wanavuliana: Ivan Rakitic (kushoto) wa Croatoa Stephane M'Bia wakibadilishana pensi zao baada ya mechi
Chukua: Rakitic na M'Bia wakiviliana nguo
Urafiki uliotukuka, hadi kubadilishana nguo za ndani
Wapinzani marafiki: M'bia na Rakitic wakiondoka pamoja uwanja baada ya Croatia kuilaza 4-0
Leave a Comment