WANANCHI WANAPASWA KUIJUA NA KUISHIRIKI BAJETI YA NCHI
NAIBUMKURUGENZI
wa Mtandao wa jinsia Tanzania TGNP Lilian Liundi amewataka watanzania kuijua
bajeti ya nchi kisera na kisekta ili iwasaidie kutathimini na kuishiriki kwa kuhoji inapokuwa haitekelezeki.
Mbali
na
hilo pia ameishauri jamii kuzielewa vema sera za kisekta nchini ili
kuwapa
uwezo na urahisi wa kutambua mafanikio na changamoto zake ikiwa ni jia
pekee ya kuharakisha upatikanaji wa maendeleo kupitia bajeti zilizopo.
Akifungua
mafunzo wanawake ngazi ya jamii na waandishi wa habari katika ofisi za mtandao
huo,Lilian alisema bajeti nyingi hazifikii malengo yake katika utekelezaji
kutokana na uelewa mdogo juu ya bajeti hizo sambamba na umuhimu wake katika
maisha ya kilasiku katika jamii.
“kumbukeni
bajeti ni moja ya rasilimali muhimu katika maendeleo katika jamii na taifa kwsa
jumla hivyo umuhimu wa kuifahamu na kuifuatilia kama inafanya kama
ilivyokusudiwa ni lazima ili tuelewe tunanini kwa ajili ya nini na imefanya
nini kwa kipindi kipi”alifafanua.
Akihimiza
jamii kuunda vikundi maalumu kufuatilia bajeti hizo alivyo vita ‘vikundi vya
mashujaa’ kufuatilia bajeti hizo, Lilian alisema jamii inapaswa kuwa mstari wa
mbele kufuatilia kwa kina ikilinganisha kiasi ilichopokea na thamani yake
kwenye utekelezaji miradi ya maendeleo.
“lakini
pia jamii inapaswa kujua kuwa ulinganifu wa kijinsia ni muhimu sana hasa katika
ufuatiliaji wa masuala haya muhimu ya kibajeti ili kupanuana mawazo katika
kukabilia changamoto zinazojitokeza’aliongeza Lilian.
Awali mkuu
wa taasisi ya mafunzo katika mtandao huo Ziki Mihyo aliwataka watanzania
hususani wanawake kutengeneza mkakati wa ushawishi na utetezi katika masuala ya
bajeti katika maeneo walipo ili utekelezwaji wake uende sambamba na matakwa ya
sera na mahitaji ya jamii.
“kila
mmoja anapaswa kutambua kuwa haki ya uchumi kwa jamii ni rasilimali zilizopo
ziwanufaishe jamii “alisema Ziki.
Jumla ya
wanawake,waandishi wa habari 35 kutoka vituo na vyombo mbalimbali vya habari
nchini wapo jijini Dar es salaam katika mafunzo ya utambuzi wa bajeti na
ushiriki wake katika kujiletea maendeleo ya kiuchumi kwenye jamii na taifa kwa
jumla.
Leave a Comment