Benki ya Dunia yaikopesha Wizara ya Fedha Bil. 498/-
Wizara ya Fedha imekoposhwa Bilioni 498 kwa ajili ya uboreshaji wa
majiji makubwa hapa nchini, kuboresha miundombinu ya maji safi na
salama, miundombinu ya maji taka, ujenzi wa vituo vya mabasi pamoja
kuboresha vichwa vya treni na reli.
Wakitia saini ya kupokea pesa hizo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr.
Servacius Likwelile alisema kuwa, pesa hizo zitatumika ipasavyo ili
kuweza kupunguza changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili sekta ya maji,
reli na majiji kuwa na miundombinu mibovu.Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kutoka nchi tatu za Afrika Tanzania, Burundi na Uganda Philipe Dongier alisema kuwa, fedha hizo zitatumika kujenga majiji mbalimbali ambayo kwa sasa yako katika hali mbaya, lengo kubwa ni kuhakikisha kunakuwa na maendeleo katika upatikanaji wa maji safi na salama, usafiri wa mabasi na treni.
Aidha Dongier alisema kuwa Benki ya Dunia itaendelea kuikopesha Tanzania katika kuhakikisha inakuwa na maendeleo hadi mwaka 2025.
Leave a Comment