Hatariiii! Mabomu Tena Arusha: Mgahawa wa Kihindi Walipuliwa na Bomu; Lingine latengwa nyumbani kwa RC

Hali ya usalama imezidi kuwa tete katika Jiji la Arusha kufuatia mfululizo wa matukio ya raia kujeruhiwa kwa kinachoaminiwa kuwa mabomu ya kurusha kwa mkono baada ya jana usiku kutokea mlipuka katika mgahawa wa kihindi ujulikanao kama Vama Restautant uliopo maeneo ya Gymkhana Jijini hapa.
Taarifa zinaeleza kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa huku wawili wakielezwa kuwa katika hali mbaya sana.
Wakati huo huo Jeshi la Polisi wakishirikiana na Askari Jeshi wamekuwa na kazi ngumu ya kutegua kinachodhaniwa kuwa bomu kilichotegwa nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa, Magessa Mulongo.
Ni wakati sasa wa vyombo vya usalama kuwa imara na kazi yao. Matukio haya ni mageni mno kwa utamaduni wa watanzania.

No comments

Theme images by sbayram. Powered by Blogger.