HII HAPA NDIYO RATIBA YA SWALA YA SIKUKUU YA IDD EL FITRI
Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ametangaza Swala ya Sikukuu ya Idd El Fitri inayotarajiwa kufanyika kitaifa katika mkoa wake.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye kikao maalumu katika Ofisi za Mkoa wa
Dar es Salaam za Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) jana, Shekhe Alhad
alisema kuwa swala hiyo sambamba na hotuba mbalimbali inatarajiwa
kufanyika saa moja asubuhi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
kutegemea na siku ya Idd itakapodondokea ambapo inatarajiwa kuwa siku ya
Jumatatu Julai 28 au Jumanne Julai 29 mwaka huu.
Shekhe
Alhad alisema kuwa swala hiyo itahudhuriwa na Rais wa Serikali ya
Jamhuri ya Tanzania, Jakaya Kikwete na viongozi mbalimbali wa Kiislamu
na wa kitaifa ikifuatiwa na Baraza la Idd litakalofanyika saa 9 Alasiri
katika Viwanja vya Karimjee, Dar ambapo Mgeni Rasmi wa Baraza hilo
atakuwa ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Peter Pinda.

Leave a Comment