Israel na Hamas watangaza kusitisha mapigano kwa masaa 12 hii leo
Jeshi la Israel na wapiganaji wa Hamas wamesema hii leo watasitisha
mapigano kwa masaa 12 kuanzia saa 2 asubuhi wakati suala la kusitishwa
kwa kudumu bado ni kitendawili kwa sasa.
Wakielezea hatua hiyo Wapiganaji wa Hamas wamesema kundi lao na
wapiganaji wengine huko Gaza wameafikiana na hoja ya kitaifa ya kujali
ubinadamu,ambapo baadaye Israel nayo ilithibitisha kuwa itasitisha
mapigano kwa kile ilichokiita ni kufungua dirisha la ubinaadamu katika
ukanda wa Gaza.
Taarifa kutoka kwa wizara ya mambo ya ndani ya kundi la Hamas huko Gaza
imetoa onyo kwa watu kutokaribia majengo yaliyolipuliwa na kambi za
kijeshi kwa kuhofia masalia ya mabomu.
Hata hivyo kuliripotiwa ghasia mapema jumamosi na kuingiza mapigano hayo
katika siku ya 19 ambapo mashambulizi ya anga ya Israel yameua
takribani watu 19 wakiwemo watoto 4 wahudumu wa afya huko gaza
wameeleza.
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry, Katibu Mkuu wa Umoja wa
Matayfa Ban Ki Moon wamekuwa katika mstari wa mbele kupata mwafaka ambao
hadi sasa haijabainika suluhu litapatikana lini.
Leave a Comment