MAFUNZO YA TIKETI ZA ELEKTRONIKI MBEYA

Na: Boniface Wambura, Dar es salaam
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeendesha mafunzo ya matumizi ya
tiketi za elektroniki kwa wadau wa mpira wa miguu mkoani Mbeya.
Mafunzo
hayo yamefanyika leo (Julai 4 mwaka huu) kwenye Uwanja wa
Sokoine, na kushirikisha wasimamizi wa mechi, viongozi wa Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA) na makatibu na maofisa habari wa
klabu za Tanzania Prisons na Mbeya City.
Wengine
walioshiriki mafunzo hayo ni Meneja wa Uwanja wa Sokoine na msaidizi
wake, wasimamizi wa milangoni (stewards) na waandishi wa habari wa
mkoani Mbeya.
Mafunzo
hayo yanahitimishwa kesho (Julai 5 mwaka huu) kwa mechi kati ya
Tanzania Prisons na Mbeya City itakayochezwa Uwanja wa Sokoine kuanzia
saa 10 kamili jioni. Kiingilio ni sh. 3,000, na tiketi zilianza kuuzwa
Julai Mosi mwaka huu kupitia M-Pesa, CRDB Simbanking na maduka ya Fahari
Huduma.
Leave a Comment