Mlipuko waua watu watano Nigeria

Boko Haram wamekuwa wakifanya mashambilizi ya mara kwa mara licha ya operesheni ya kijeshi dhidi ya wapiganaji hao
Takriban watu watano wameripotiwa kuuawa katika mlipuko uliotokea sokoni Maiduguri kaskazini mwa Nigeria.
Watu
walioshuhudia tukio hilo wameiambia BBC kuwa gari lililokuwa limebeba
mkaa lilipuliwa na bomu linalodhaniwa liliwekwa ndani ya gari hilo.
Hadi sasa hakuna kundi lolote la kigaidi lililokiri kuandaa shambulio hilo.
Tukio
hili linakuja huku ripoti ya hivi karibuni ya jeshi la Nigeria ikisema
kuwa limeshambulia moja ya ngome za kundi la wapiganaji la Boko Haram.
Mwandishi
wa BBC Habiba Adamu toka mji mkuu wa Nigeria Abuja aliyetembeela eneo
hilo anasema kuna utata wa idadi ya waliouawa katika shambulio hilo
kwani wakati wengine wakisema waliouawa ni watano wengine wanasema
huenda idadi ya waliouawa ikawa ni zaidi ya hiyo iliyotolewa.
Leave a Comment