PICHA: SAFARI YA MWISHO YA MWANAFUNZI DANIEL LEMA ALIYECHOMWA MOTO KWA KUTUMIWA KUWA MWIZI
Mwili
wa Daniel Lema ukiagwa na baadhi ya wanachuo pamoja na raia
waliojitokeza kuhudhuria ibada ya kuuaga mwili wa marehemu mapema
asubuhi ya leo katika hospitali ya rufaa mkoani iringa.
![]() |
| Mwanafunzi (LEMA) aliyejeruhiwa kwa moto |
LEMA
Aliyekua akisoma mwaka wa 4 kozi ya sheria katika chuo kikuu kishiriki
cha Mt.Augustino Tawi la Iringa (Ruaha University College-RUCO),
mwanzoni mwa wiki hii ameshambuliwa kwa kuunguzwa na moto akidhaniwa ni
mwizi.
Mnamo
tarehe 24.06.2014 mwanafunzi huyo alikua ametoka kuangalia michuano ya
kombe la dunia na akiwa amelewa akawa anatafuta chakula cha jioni na
ilikua majira ya saa 5 Usiku, Mwanafunzi huyo aliingia kwenye mgahawa
ambao biashara ilikua imefungwa kwa muda huo lakini ndani kulikuwapo na
binti ambaye alianza kupiga kelele kwa kudhani alikua mwizi.
Na kwakua eneo hilo kulikuwa na mlinzi(Mmasai) ndiye aliyeanza kumshambulia mwanafunzi huyo.
Baada
ya tukio hilo wakatokea watu (2) waliojitambulisha kuwa ni askari
wakaamuru mwanafunzi huyo asipigwe kwa madai ya kumfikisha kituoni.
Lakini
baada ya mwendo mfupi kuelekea kituoni mwananchi mmoja alimchukua
kijana huyo kinguvu kisha kumwagia mafuta na kisha kumuwasha moto, ambao
ulizimwa na madereva bodabora walio kuwa eneo hilo na kisha kumkumbiza
kijana huyo hospitali.
Mpaka sasa Kijana huyo amelazwa katika
wodi ya watu mahututi (ICU) katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa
ambapo mama yake mzazi pamoja na kaka yake ndio wanaomsaidia
kumuhudumia.
Mwili wake umeagwa mapema leo katika
hospitali ya rufaa mkoani Iringa tayari kwa safari ya kuelekea mkoani
Kilimanjaro kwaajili ya mazishi yatakayofanyika siku ya juma tano.
Lema alizaliwa mnamo tarehe 05/06/1989 na kufariki tarehe 30/06/2014 Mungu na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi!!!


Leave a Comment