TACAIDS YAKIRI KUPUNGUA KWA MAAMBUKIZI YA UKIMWI NCHINI
Afisa
Mawasiliano Kutoka TACAIDS Bw. Godlease Malisa akizungumza na waandishi
wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari
uliofanyika katika banda la TACAIDS kwenye viwanja vya Sabasaba jana
Jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini
kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr. Jerome Kamwela.
Mkurugenzi
wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr.
Jerome Kamwela akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa
habari uliofanyika katika banda la TACAIDS kwenye viwanja vya Sabasaba
jana Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Mawasiliano Kutoka TACAIDS
Bw. Godlease Malisa.
Mkurugenzi
wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr.
Jerome Kamwela kati akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa wa Ufuasihii
wa dawa na huduma za jamii wa ICAP Globali Health Action Bi: Agnes
Rubare Rwegasha alipotembelea banda la ICAP, kushoto ni Afisa
Mawasiliano Kutoka TACAIDS Bw. Godlease Malisa

Jerome Kamwela akimuuliza swali Mwelimisha Rika kutoka PSI (Population
Service International) Bi: Veronica Mbilinyi alipotembelea banda hilo
katika Viwanja vya Sabasaba leo jijini Dar es Salaam.
Na Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikali – WHVUM
Tafiti zilizofanywa na Tume ya
Kudhibiti Ukimwi Tanzania zinaonyesha kuwa maambukizi mapya ya Virusi
vya Ukimwi nchini yamepungua hadi kufikia asilimia....
5.1 kwa mwaka
2011/2012 ambapo asilimia 6.2 ni wanawake na asilimia 3.8 ni wanaume.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi
wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr.
Jerome Kamwela jana katika Viwanja vya Sabasaba alipokutana na waandishi
wa Habari katika banda la TACAIDS kuwaelezea hali halisi ya maambukizi
mapya ya Virusi vya Ukimwi nchini.
Dr. Kamwela amesema kuwa TACAIDS
imekua ikifanya ukaguzi wa tafiti (takwimu) zilizokusanywa katika maeneo
mbalimbali nchini na kuzitathmini tafiti hizo kama zina viwango wakiwa
na lengo la kupanga mikakati itakayowawezesha kuelekeza rasililmali ili
kuondoa maambukizi mapya yanayoweza kujitokeza.
“Tafiti zinaonyesha kuwa Mkoa wa
Njombe unaongoza kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa asilimia 14.7
ambapo Iringa ina asilimia 9.1 ya watu walioathirika na Virusi vya
Ukimwi na Mbeya ikiwa na asilimia 9, kwa upande wa mikoa yenye kiwango
cha chini cha maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ni Manyara na Kilimanjara
ikiwa na asilimia 2 ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi” amesema Dr.
Kamwela.
Akizungumzia kuhusu changamoto
ambazo TACAIDS imekua ikizipata katika ukusanyaji wa takwimu za watu
wanaoishi na Virusi vya Ukimwi nchini Dr. Kamwela amesema kuwa uhaba wa
wataalamu, uhaba wa vyuo vinavyofundisha taaluma ya ufuatiliaji na
tathmini pamoja na uhaba wa fedha kwaajili ya kufuatilia na kutathimini
hali halisi ya maambukizi ya Ukimwi nchini vimekua vikizuia malengo ya
kutokomeza Ukimwi nchini.
Kwa upande wake Afisa Mawasiliano
kutoka TACAIDS Bw. Godlease Malisa amesema kuwa TACAIDS imekuja na
mkakati unaozingatia sifuri tatu (three zeros) ukiwa na maana sifuri ya
kwanza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi yashuke hadi sifuri, huku
sifuri ya pili ikimaanisha unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na Virusi
vya Ukimwi upingwe hadi sifuri na sifuri ya tatu ikimaanisha maambukizi
ya mama kwenda kwa mtoto yapunguzwe hadi sifuri.

Leave a Comment