WAANDISHI KUNOLEWA VITA DHIDI YA UPANGAJI MATOKEO

Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Taasisi
moja kutoka Uingereza inayohusika na kampeni dhidi ya upangaji matokeo
kwenye mpira wa miguu (match fixing) itafanya uwasilishaji
(presentation) juu ya suala hilo kwa waandishi wa habari za michezo
nchini.
Uwasilishaji
huo utafanyika kesho (Julai 5 mwaka huu) saa 11 jioni kwenye hoteli ya
Accomondia iliyopo Barabara Nkrumah jijini Dar es Salaam.
Wataalamu
hao wa kupiga vita upangaji matokeo ambao pia wataelezea jinsi matokeo
yanavyopangwa, jana (Julai 3 mwaka huu) walifanya uwasilishaji wao kwa
wachezaji na benchi la ufundi la timu ya Taifa ya vijana wenye umri
chini ya miaka 17 (Serengeti Boys).
Taasisi
hiyo yenye kibali kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) katika utoaji elimu ya kubaini upangaji matokeo, vilevile inatoa
elimu juu ya athari zinazopatikana kutokana na upangaji matokeo.
Leave a Comment