Wanne wafariki dunia katika ajali ya ndege Nairobi
Watu wanne wamefariki dunia asubuhi ya leo na wengine kadhaa kujeruhiwa
baada ya ndege ya mizigo iliyokuwa ikielekea mji mkuu wa Somalia,
Mogadishu kugonga jengo la kibishara katika eneo la Embakasi, baada ya
kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini
Nairobi.
Joseph Ngisa Mkuu wa Upelelezi katika Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa
Jomo Kenyatta (JKIA) amesema kuwa, uchunguzi wa mwanzo umeonesha kuwa
ndege hiyo ilikuwa inapaa katika masafa ya chini baada ya kutoka
uwanjani na kwamba iligonga mlingoti wa umeme kabla ya kuanguka.
Waliofariki dunia kwenye ajali hiyo ni watumishi wanne waliokuwa ndani ya ndege hiyo ya mizigo aina ya Fokker 50.
Maafisa wa Kenya wamesema kuwa, uchunguzi bado unaendelea ili kubaini chanzo kikuu cha ajali hiyo.

Leave a Comment