HATUA 5 ZA KUZUNGUMZA NA MPENZI WAKO ALIYEKASIRIKA
Kwenye mapenzi kuna nyakati za kutofautiana
au kukasirishana, Katika hali ya kawaida kipindi hiki huwa ni cha hatari kwa
sababu husababisha nyufa kubwa za uhusiano na kulifanya penzi kukosa ladha.
Sote tunajua, watu hupigana, huachana, hujeruhiana, hutukanana, hudhalilishana wakiwa na hasira. Hata hivyo si wote wanaojua wafanye nini wanapojikuta wameingia kwenye hatua hiyo mbaya
.Sote tunajua, watu hupigana, huachana, hujeruhiana, hutukanana, hudhalilishana wakiwa na hasira. Hata hivyo si wote wanaojua wafanye nini wanapojikuta wameingia kwenye hatua hiyo mbaya
Hebu jaribu kukumbuka ugomvi mmoja uliotokea kati yako na mpenzi wako na ikiwezekana jikumbushe mlivyoanza! Utabaini kuwa mlianza kama utani na mkajikuta mmefura kwa hasira, mkatwangana makonde, mkatamkiana maneno makali ya kuudhi na pengine mkaamua kuachana.
Yote hii ni kwa sababu mlikosa elimu ya
mazungumzo. Ingekuwa mmoja wenu hasa yule aliyekuwa wa pili kukasirika anafahamu
hatua za kuzungumza na mtu aliyekasirika angechukua jukumu la kutuliza
machafuko na kuleta amani kwenye mapenzi. Tazama hatua tano za kuzungumza na
mpenzi aliyekasirika.
1.MPUNGUZE
MHEMKO
Hasira hujaza kifua, huathiri mzunguko wa
damu na ufahamu. Mtu aliyekasirika huwa vigumu kwake kusikiliza au kutazama
mambo kwa jicho la tatu. Mwenye hasira huwa hafikirii matokea yajayo badala
yake hutazama zaidi tukio na jinsi ya kupata ushindi iwe kwa maneno au kwa
mapambano.
Katika hali ya namna hiyo, mtu mwingine akija na busara za kutaka kumgeuza haraka haraka hawezi kumuelewa. Muhimu hapo ni kuacha kumwadama, kujibizana naye, kumshawishi asikilize badala yake mpe nafasi ya kusema atakavyo, abwate ajuavyo huku wewe ukimuitikia na kumkubalia lawama zake.
Katika hali ya namna hiyo, mtu mwingine akija na busara za kutaka kumgeuza haraka haraka hawezi kumuelewa. Muhimu hapo ni kuacha kumwadama, kujibizana naye, kumshawishi asikilize badala yake mpe nafasi ya kusema atakavyo, abwate ajuavyo huku wewe ukimuitikia na kumkubalia lawama zake.
Hivyo mtulize na kauli kama hizi “Basi mpenzi mwenye makosa ni mimi.”
Kauli za aina hii zitampunguza hasira kwani atajiona mshindi.
2.MSOME
SAIKOLOJIA YAKE
Kwa kuwa unamfahamu mpenzi wako kwa kina
itakuwa rahisi kwako kumtambua kuwa amepunguza hasira na kurudi katika hali
yake ya kawaida. Ukisha fahamu hilo chukua jukumu la kumsoma kisaikojia ili
kujua kama yuko kwenye hali nzuri ya kusikiliza yale uliyotaka kumwambia wakati
alipokuwa na hasira.
Zoezi hili linaweza kuchukua saa kadhaa na
wakati mwingine hata siku mbili. Lengo ni kupata matokeo sahihi ya kuondoa
chuki za mwenza wako na kumfundisha madhara ya kukasirika kwenye uhusiano wenu
wa kimapenzi. “Mpenzi, nakupenda sana,
lakini juzi uliniumiza, uliniambia mimi malaya kwa kosa ambalo sikufanya”
Bila shaka muda huo atakusikiliza zaidi kuliko ungebishana naye alipokuwa na
hasira.
3.MRUHUSU
AKUJIBU
Pamoja na kumsoma kisaikojia na kumwambia
kinagaubaga makosa yake, usimzuie kujitetea, mpe nafasi ya kuzungumzia
kilichomkasirisha, mwache ajibu hoja hata kama atakuwa anakukandamiza na kuzidi
kujijengea ushindi.
4.EPUKA
MARUMBANO
Kama nilivyosema, wapenzi wengine huwa
wagumu kuelewa, ni watu wa kuficha udhaifu wao na kutopenda kuonekana
wamekosea. Watu wa namna hii unapowarejeshea mazungumzo wanaweza kujikuta
wanahamaki tena.
Watakuwa na kauli hizi “Kwa hiyo ulikuwa unasemaje…nilifanya
ndiyo,… wewe unaamuaje?” Mkifika
kwenye alama hiyo usikubali kurumbana naye mwache aseme halafu wewe ingia kwenye
hatua ya tano.
5.MUOMBE
MSAMAHA
Hata kama atakuwa yeye ndiye mwenye makosa
na amekataa kukiri, usijali, chukua jukumu la kumuomba msamaha na kueleza tena
nia yako ya kimazungumzo ilikuwa ni kuelewana si kugombana.
Kumbuka hata kama amekiri kosa, bado unatakiwa
kumuomba radhi kwa kurejea yaliyopita. “Mpenzi
inawezekana nikawa nimekuudhi kwa niliyosema, nakuomba sana tusameheane.”
Bila shaka kwa haya machache utakuwa umejifunza na kuchukua hatua za kuzuia migogoro mikubwa inayotokana na hasira za mpenzi wako.

Leave a Comment