NJIA NNE ZA KUFUFUA PENZI LILILOCHOSHA

Watafiti wa masuala ya kimapenzi tunaamini
kwamba, mvuto wa mapenzi miongoni mwa wapendanao hupungua kadiri siku za
uhusiano wao zinapokuwa nyingi, ushahidi unapatika kwa takwimu za usaliti kuwa
chini ya asilimia 13 kwa mapenzi yenye muda wa kuanzia mwezi mpaka mwaka mmoja.
Inabainishwa kuwa kiwango cha watu
kusalitiana hupanda sambamba na umri wa uhusiano wenyewe. Katika uchunguzi
wangu nimebaini kwamba wanawake wengi hawasaliti ndoa zao katika kipindi cha
uhusiano mchanga na kwamba huwa tayari kuvunja uhusiano na wapenzi wao wa
zamani kwa lengo la kulinda penzi jipya.
Lakini upo ushahidi wa wengi kuanza
kurejesha uhusiano waliokufa, pindi wanapoishi na wenza wao kwa muda mrefu
kiasi cha kuzoeana sana. ( Nidokeze tu kwamba kuna wadanyanyifu wa mapenzi
ambao husaliti ndoa hata siku ya harusi yao, hawa tutazungumzia habari zao
wakati mwingine). Hali hii hutokana na kukinaishwa na penzi la wapenzi wao na
hivyo kuhitaji mshawasha mpya.
Kushuka kwa msisimko wa kimapenzi kuna
dalili nyingi lakini kubwa kati ya hizo ambayo ndiyo huwasumbua wengi hasa
wanaume ni kushindwa kufanya tendo la ndoa na wenza wao au kutenda na kupata
starehe chini ya kiwango. Kwa kipindi cha miezi minne nimepokea kesi zaidi ya
81 kutoka kwa watu mbalimbali zikieleza kuwa wamepoteza hisia za kimapenzi kwa
wapenzi na wanandoa wao.
Jambo kubwa katika tatizo hili ni matokeo
baada ya watu kupatwa na hali ya kupoteza hisia za mapenzi. Wengi wao wamekuwa
wakiamua kuachana na wenza wao na kuanzisha uhusiano mpya kwa msukumo wa hisia
kali za mapenzi machanga ambazo walikuwa nazo hata walipokutana na wale
wanaoachana nao.
Kitalaamu ukitafsiri uamuzi huo, unapata
kasoro za ufahamu ambazo zinahitaji elimu.
Watu wengi wamekuwa wakiuliza, wanaweza
kufufua penzi lililokinai? Jibu ni kwamba wanaweza, endapo watafuata mambo
yafuatayo kwa vitendo.
1.KWANZA ni kujenga
ufamilia na umpendaye, nikiwa na maana kwamba awe rafiki na mtu wako wa karibu
katika matembezi na maongezi. Wengi tunakutana na wenza wetu wakati wa kulala,
sasa huo msisimko wa kimapenzi utapatikana wapi katika mazingira haya?
2.PILI, ni kumthaminisha
mwenza wako kwa ubora kila wakati. Msisimko wa kimapenzi hauweza kuja kama
hujavuta hisia juu ya jambo au maumbile fulani ya mwenza wako. Inashauriwa kila
mara umtazame mpenzi wako kwa kumtathimini vema na kujivunia, miguu yake ya
bia, umbo namba nane, kasheshe zake faragha na mvuto wake kwa ujumla. Ukiwa na
vitu hivi vitakusaidia katika kuzalisha homoni na kukuza hisia zako.
3.TATU ni kuwa na kitu
kinachoitwa uchumi wa kimapenzi ambao hutokana na kumfikiria mpenzi wako kila
mara unapokuwa kazini, kwenye matembezi na ikiwa unaona vitu barabarani au
kwenye maduka jaribu kuwaza au kuvinunua kwa ajili ya kukuza penzi lako. Hapo
utafanikiwa kukuza penzi.
4.NNE na la mwisho ni kuazima hisia. Kwa mfano unaweza usiwe na msisimko na mpenzi wako lakini ukawaza mwanaume mwingine na kumfananisha na uliyenaye, hili si jambo baya na linatajwa kusaidia kuamsha penzi lililokinai.
Kama hilo halitoshi kuazima hisia
kunakwenda mbali hadi kwenye kupokea sifa toka kwa rafiki zako zinazomhusu
mwenzako, mfano. “Mume wako mpole anavutia kweli” Kauli hizi ukizitafakari
zitakusaidia kufufua mapenzi yako.
Leave a Comment