RAIA WA VIETNAM AKAMATWA NA MZIGO WA MENO YA TEMBO NA KUCHA ZA SIMBA WENYE THAMANI YA MIL 189,420,000.
Jeshi
la Polisi linamshikilia Raia wa Vietnam Dong Van(47) kwa kumkamata
akiwa na meno 65 na kucha 447 za Simba kinyume cha sheria vyenye thamani
ya Shilingi Milioni 189,420,000.
Kamishna
Msaidizi wa Polisi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, Hamisi Selemani, amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa jana wakati
alipotaka kusafirisha nyara hizo kwa kutumia Shirika la Ndege la Qatar
Airways kwenda nchini Vietnam kupitia Doha.
Amesema alipopekuliwa alikutwa na nyara hizo ambazo alizihifadhi kwenye
pakiti 7 za kahawa na pakiti moja ya mchele na kuzichanganya na pakiti nyingine 15 za vyakula vya aina mbalimbali
Kamanda
Selemani amesema pakiti hizo ziliwekwa ndani ya begi la nguo ili
kupoteza ushahidi wa aina ya mzigo alioubeba kwa wakaguzi wa uwanjani
hapo.
Aidha amesema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Bado una haki ya kupata habari kila ikinifikia cha msingi ni ku-like ukurasa wangu wa facebook Mr. Clever Blog

Leave a Comment