Alshabaab wamteua kiongozi mpya
Aliyekuwa kiongozi wa Al Shabaab Ahmed Godane
Kundi la wanamgambo la Al Shabaab limemtaja kiongozi wao
mpya, baada ya aliyekuwa mwanzilishi wa kundi hilo Ahmed Godane kuuawa katika
shambulizi lililofanywa na majeshi ya Marekani wiki ya jana.
Kiongozi
huyo mpya wa sasa ni Ahmad Umar, ambaye kwa mujibu wa kamanda wa Al Shabaab Abu
Mohammed, amesema uamuzi wa kumteua kiongozi huyo ulifikiwa bila pingamizi.
Katika
taarifa ya kundi hilo, ilionya kutaka kulipiza kisasi mauaji ya kiongozi wao,
na kusema hilo ni jukumu la Al Shabaab ambalo hawatawahi kukosa kutekeleza azma
hiyo.
Aidha,
mapema siku ya jumapili, waziri wa usalama wa ndani wa Marekani,amesema serikali
yake imepokea taarifa za kundi hilo kupanga kushambulia vituo vya afya, elimu
na taasisi zingine za serikali nchini humo.
Leave a Comment