ANGALIA PICHA, PAKA AFUNGWA BONGE LA HIRIZI SHINGONI JUU YA MTI KARIBU NA MSIKITI MOROGORO

Paka
mwenye hirizi kubwa shingoni akiwa amepigiliwa misumari juu ya mti
uliopo jirani na Msikiti wa kwa Mtawara uliopo Kata ya Mwembesongo,
Morogoro.
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida, paka mwenye hirizi kubwa shingoni akiwa hai
alikutwa amepigiliwa misumari juu ya mti uliopo jirani na Msikiti wa kwa
Mtawara uliopo Kata ya Mwembesongo mkoani Morogoro.
Tukio
hilo lililokusanya umati mkubwa wakiwemo waumini wa msikiti huo
lilitokea alfajiri ya Alhamisi iliyopita ambapo baadhi ya waumini wa
msikiti huo walikuwa wamefika msikitini kwa Swala ya Alfajiri.
Baadhi
ya waumini wa msikiti huo walipohojiwa na mwandishi wetu walisema
alfajiri hiyo walisikia sauti ya paka akilia kutoka kwenye mti huo
uliopo kandokando ya Barabara ya Mtawara inayoelekea Kichangani na Mji
Mpya.
“Tulifika
hapa msikitini kwa lengo la kuswali Swala ya Alfajiri kwa kuwa bado
kulikuwa na giza hatukuweza kumwona, lakini tulisikia akilia kwa kupiga
kelele mfululizo.
“Tuliposogelea
tulimwona akiwa juu ya mti huku amevishwa hirizi kubwa ya rangi nyeusi.
Haya ni mambo ya kishirikina, tena tuna wasiwasi hata wa maisha yetu.
“Unajua
eneo hili lina miti mingi lakini wahusika wamekuja kumpigilia misumari
paka huyu hapa. Mimi nasema wasakwe hawa watu tuwajue,” alisema muumini
mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah Said.
Naye mjumbe wa kamati ya utendaji ya msikiti huo, Haji Said Dihole alipohojiwa na mwanahabari wetu alisema:
”Kama
kuna mtu alitaka kutujaribu angemuweka paka huyo kwenye eneo letu la
msikiti angeipata habari yake, pia nasikia tukio kama hili liko kwa
majirani wetu pale Kanisa la T.A.G Mwembesongo, nenda kashuhudie.”
Paka huyo baada ya kutolewa mtini.
Baaada
ya kupata taarifa hizo, mwandishi wetu alifunga safari hadi kwenye
Kanisa la Tanzania Assemblies of God ‘T.A.G’ linalofahamika kwa jina la
Bethel Revival Temple lililopo Mwembesongo.
Mwandishi
wetu hakumkuta paka lakini wananchi wa eneo hilo walipoulizwa walikiri
kuwepo kwa paka huyo kwenye mtaa huo lililopo kanisa hilo lakini
aliondolewa.
Leave a Comment