HIZI NDIO FAIDA KUMI(10) ZA HUGGING (KUKUMBATIA), ANZA LEO
1.Husaidia uzalishaji wa homoni ya “oxytocin” ambayo husaidia sana mwili kuondoa tatizo la kuhisi upweke, hasira, na kutengwa.
2.Unapomkumbatia mtu, unaupa mwili hali ya kujihisi salama na huru pia.
3. Hug hufanya misuli isinyae hivyo kusaidia kuondoa/kupunguza baadhi ya maumivu ya mwili na kuufanya uwe huru.
4.Huboresha mahusiano ya watu wanaopendana kwani unapomkumbatia mtu unaonyesha hali ya kupenda, usalama, na mapenzi ya dhati.
5.Huondoa uoga na wasiwasi.
6.Utajikuta
unajiona wa thamani kumbuka tulipokuwa wadogo, wazazi wetu
walitukumbatia na tukajiona tunapendwa na tuko mahali salama, upendo ule
tulioonyeshwa na wazazi wetu, unakuwepo ndani yetu kadri tunavyokuwa
watu wazima, na unapomkumbatia mtu inakufanya uhisi kupendwa na
wathamani.
7.Huleta
usawa kwenye Mfumo wa fahamu kwani wengi wetu tunaishi katika mazingira
yanayoufanya mwili kuwa katika hali ya kujihami muda wote hivyo
unapomkumbatia mtu, mwili husinyaa na kurudi katika hali yake ya
kawaida.
8.Hug hutufundisha kutoa na kupokea.
9.Hushusha
shinikizo la damu mwilini, Mgusano wa mwili husababisha neva za kwenye
ngozi zinazoitwa “Pacinian corpuscles” kupeleka habari kwenye sehemu ya
ubongo (vagus nerve) inayohusika kushusha shinikizo la damu.
10.Watoto
wanaokumbatiwa kwa kiasi kikubwa wakiwa watoto, huwa katika hatari
ndogo zaidi ya kupata msongo wa mawazo kuliko watoto wasiokumbatiwa vya
kutosha.

Leave a Comment