JINSI YA KUMVUMILIA MPENZI WAKO NA MAPUNGUFU YAKE
Leo naomba tuzungumzie kitu ambacho ni
muhimu sana kwa mahusiano na ndoa pia. Unapojiandaa kuingia katika ndoa
unapaswa kujiandaa jinsi utakavyokwenda kuishi na mwenzi wako. Maana uhusiano
unaouendea sio kama ule uliokuwa nao na Baba, Mama, kaka, dada au bibi yako, ni
Zaidi sana mpendwa, unaingia katika uhusiano wa karibu wa ndani mtu ambaye
utalala naye kitanda kimoja kila siku na wakati.
Ni mtu ambaye iwe jua iwe mvua
utakuwa unamuona.
Mtu ambaye hata kama hujisikii
kuongea na mtu siku hiyo atakuongelesha
Mtu ambaye hata kama hujisikiaa
kumuona atakuwepo hapo na utamuona
Ni mtu ambaye lazima uwe naye karibu
hata kama siku hiyo amekukwaza sanaa
Ndio maana tukaona kuna umuhimu wa
kuwa na masomo haya maana mengi yametokea kama tunavyoona katika jamii sasa,
talaka sasa inatolewa kirahisi rahisi tu.
Kuhusu kuchukuliana ni hali ya kumuelewa mwenzako pale
anapofanya kitu ambacho hakikufurahishi au usichokipenda.
Lakini kuchukuliana sio kupuuzia au kudharau naomba
nitofautishe maana wengi wanapuuza au kudharau mambo wenzao wanayoyafanya hiyo
nayo yaweza kuleta shida.
Ukimchukulia mtu utaona mazuri
badala ya mabaya, utaona upande wake mzuri Zaidi ya ule mbaya. Najua utaniuliza
kuna mtu mbaya kweli? Ni kweli kabisa kila mtu ana sehemu mbili za maisha ana
upande chanya na hasi au ana upande wa mazuri na madhaifu, kila mwanadamu ana
pande zoote hizo wala usije ukafikiri ni wewe mwenyewe.
Zamani nilikuwa nasema ukiwa na
mahusiano na mchungaji au shehe maana wao ni watumishi wa Mungu hawana shida,
lakini hata awe askofu, Nabii, Mpakwa Mafuta, ana pande mbili nzuri na madhaifu
maana yeye ni mwanadamu. Ni Mungu tu anatupa nguvu ya kushinda katika madhaifu
yetu.
Sasa kama mwenzako atakuwa na kitu
ambacho hakikufurahishi na umeshamwambia weee na habadiliki ni jukumu lako Kumuelewa, Kumuombea na KUMCHUKULIA yaani
hapo utakuwa na ndoa yenye ushindi hapa duniani, furaha na raha zitakuwa ni
sehemu ya maisha yenu.
Kama mwenzako ana tabia za Ujeuri,
mwelewe kwanza hii tabia imeletwa na nini maana kuna wakati unaweza kuwa wewe ndio
chanzo cha tabia mbaya kwa mwenzako, lakini pia nyingine ni malezi aliyokuwa
nayo.
Kuna mtu ninamjua amelelewa katika
familia yenye wakaka wengii sana, yeye akiwa mtoto wa kike peke yake kwahiyo
hata kuongea na vitabia fulani ni vya kiume kiume, sasa mume atakayemuoa
asipomuelewa huyu dada itakuwa ni mtihani maana anaweza kuongea kitu cha kisela
sela mume akaona hivi nimeoa mwanaume mwenzangu au? Lakini atakapoelewa kwamba
hii ni adhari ya mazingira mwenzi wangu aliyokulia itakuwa ni faida kwa wote maana
ataweza kumsaidia mwenzake na pia atamchukulia pindi tabia ile ya kibabebabe na
kisela inajiinua lakini asipomuelewa hiyo ndoa itakuwa na shida sana.
Lakini pia ukiona mwenzako
anashindwa kukuelewa mwambie mbona mimi naona kawaida kwasababu nilizoea kuongea
hivyo na ndugu zako sasa sikuwahi kuambiwa kama ni shida basi kama kwako ni
shida nitaacha naomba Mungu anisaidie.
Sasa kama wewe unajifanya ni mtu wa
sheria sheria unataka mwenzako atembelee katika chaki utapata shida sana katika
ndoa, kwasababu kwanza hakuna mtu aliye mkamilifu na pili mwenzako ataishi kwa
uwoga sana na wewe atakuogopa mnoo. Sasa akikuogopa ni hatari kwa ndoa maana
kuna mambo mengi yake ya muhimu hutayajua na anaweza kujaribiwa kuwa na
marafiki wa nje.
Kuna mtu alisema yeye alilelewa
katika mazingira ya mpangilio sasa alivyooa mke wake akawa ni mtu ambaye
kwakweli anaweka vitu hovyohovyo, sasa yule kaka akawa anakwazika sana sana
akawa anamwambia mwenzake wewe ni mtu wa aina gani unakuwa haufanyi vitu kwa
mpangilio?
Mwenzake naye akawa anakwazika mbona
huyu ana Maneno makali mbona mimi nimekaa kwetu miaka 20 plus hakuna hata ndugu
yangu mmoja alinisema hivyo sasa hilo swala likaleta shida kubwa katika ndoa
hiyo, kukawa hakuna maelewano ndani ya ndoa , ndio huyu mkaka kwa hekima ya
Mungu akajitenga akamuomba Mungu , ndipo Mungu akamfundisha kuchukuliana na
mwenzake, na ndoa ikasalimika. Niliweza kumuona akitoa ushuhuda hapa
nimefupisha ila kuchukuliana kuliokoa sana ndoa yao.
Kama ndio mko katika uchumba anza
kumuomba Mungu akusaidie uweze kuchukuliana na mwenzako.
Namna ya kujifunza Kuchukuliana na
mwenzi wako;
Ili kuchukuliana na wenzako iwe
sehemu ya maisha yako unahitaji kujifunza kwa njia zifuatazo;
1.Anza
kuchukuliana na ndugu zako, wadogo zako na jamaa zako
2.Chukuliana
na wanafunzi wenzako kama uko chuo
3.Jifunze
kuchukuliana na room mate wenzako kama uko chuo
4.Chukuliana
na wapangaji wenzako kama umepanga nyumba ya watu wengi
5. Chukuliana
na washirika wenzako kanisani
6.Jinfunze
kuchukuliana na wafanyabiasha wenzako
7.Popote
ulipo ukatukatana na mtu akakukwaza jitahidi kumchukulia
Ukijifunza hayo
utakuta umeifanya ikawa tabia yako yaani utajikuta unawachekea na kuwafurahia
wale wanaokukwaza na utaishi maisha ya ushindi ambayo Mungu ametukusudia tuishi
hapa duniani.
Leave a Comment