Mahusiano ya kimapenzi ni kama moto wa kuni!!!!
Unaweza
ukajiuliza kwanini ninasema hivyo usipate jibu, au ukapata majibu
tofauti na haya niliyo nayo katika makala hii ya mahusiano.
Kwa
wale wenye kufahamu moto wa kuni ni mto mzuri sana kwa mapishi na
wanawake wa vijijini wanajua raha ya moto huo, unaivisha mapema, hauna
gharama kubwa kama mkaa, gesi, umeme, mafuta ya taa na nishati
nyinginezo.
Kama ilivyo kawaida hakuna kilichokuwa na raha kikakosa karaha, ingawa karaha zinazidiana kulingana na kitu husika.
Moto
wa kuni una moshi mwingi hasa ukikuta kuni mbichi, unasumbua kuwaka na
kupuliza ni sehemu ya kuuchochea moto huu, wengine hadi macho hubadilika
na kuwa mekundu kwa ajili ya moshi, taya nazo uuma kwa sababu ya
kupuliza moto na vikamasi vepesi navyo huwa karibu haya yote ni ili
chakula kiive mapema ndiyo maana nasema mahusiano ya mapenzi ni sawa na
mto wa kuni.
Katika
mahusiano ya mapenzi kuna bashasha nyingi ambazo zinahitajika ili
kuendelea kuimarisha mahusiano yako ya kimapenzi na Yule umpendae na
karaha nyingi ambazo huwafanya baadhi ya wanandoa kukata tamaa na
kuwashawishi wengine kutodhubutu kuingia kwenye ndoa.
Bila
kujua wapi alipokosea na nini anapaswa kufanya ili kuwa katika hali ya
mahusiano imara yenye maisha ya umilele, kudhani suluhisho ni kuachana
na mume au mke wake.
Kazi
hii si ya mtu mmoja bali ya wote wawili ingawa watu wengine, hawana
utamaduni wa kujua nini mwezake anahitaji na amtimizie kwa wakati gani
na wapi alipokosea.
Ila
ukweli usiyo pingika kuwa kama utapenda kutumia jiko la kuni lazima
ukubali karaha zake na raha zake, na mahusiano yako ili yawe imara
lazima uwe mwepesi wa kupenda kufanya yale mwezako anayokufanyia kwa
maana kuwa inawezekana anapenda umfanyie ila anaona haya kukwambia.
Watu
wametofautiana kimaumbile mpaka tabia hivyo, mapenzi siku zote hayataji
ujuaji mwingi sana, ila yanataka ubunifu kama jiko la kuni, sasa kuna
jiko la ukuni mmoja na kuna la kuni tatu, huu ni ubunifu wa jiko la
kuni.
Jifunze
kujinyima kwa ajili ya mume wako au mke wako ili kufanya angalau kitu
kimoja ambacho kitakuwa cha kipekee sana katika mahusiano yenu na
kitaendelea kuwa kumbukumbu isiyofutika.
Kuna
jamaa mmoja wa huko uhaibuni alikuwa anatamani sana kumfanyia mambo
mengi mke wake, lakini hakuwa na uwezo wa kufanya hivyo, alikusanya
shilingi hamsini kwa kila siku
baada ya miaka kumi alikuwa anahela nzuri tu akaenda kumnunulia mke wake
zawadi ambayo ilimfariji sana mkewe na kujiona kama vile ndiyo
anachumbiwa.
Je
wewe unafanya nini ili kuwa na mahusiano yenye kumbukumbu nyingi katika
maisha yenu ya ndoa au umeridhika kwa kuwa umeshaoa au kuolewa?
Nawapongeza
sana wanawake waliyo wengi ni hodari sana katika kuhakikisha
wanawanunulia weza wao, zawadi mbalimbali, hata kama hana kazi atakuomba
hela kwa madai ya kuwa na shida Fulani ili aweze kukununulia zawadi.
Lakini
baadhi ya wanaume hujifunza na kuanza kufanya hivyo, na wengine hupuuza
na kuona kama kuni mbichi ambazo hata uchochee bado zitatoa moshi.
Maisha
ya mwanamke siku zote yamekuwa ya kipekee sana katika ndoa ingawa pia
huingiliwa na mtihani wa ushindani wa kutaka kuwa wakipekee sana katika
mahusiano.
Wanawake
wengi wanakuwa wanachoka kwa kuona pengine zawadi anazotoa kwa mumewe
hazifirahii na ndiyo maana anahindwa kujibu kwa kumpa na yeye zawadi.
Kwa
hakika zawadi ni moja ya kichochezi kikubwa cha kuweza kumweka mtu
aliye mbali karibu kimwili na hata kiakili na hii huwa kama deni ndani
ya dhamira ya anayetoa kumbuka ukijua kupokea jua na kutoa.
Hiyo
ni misemo ya zamani ila ina maana kubwa sana endapo utataka kujua maana
yake je wewe umepokea mara ngapi vingapi umerudisha?
Leave a Comment