MASWALI YA KUULIZANA WANANDOA WATARAJIWA KABLA YA KUOANA



Wanandoa watarajiwa walio wengi hufanya maandalizi makubwa ya sherehe ya harusi kuliko maandalizi ya kuishi maisha mapya wanayoyaendea. Ingawa si wote wanaweza wakawa wawazi/wakweli lakini ni vyema ukajiulizana maswali yafuatayo kabla ya kuingia kwenye ndoa:-
1. Kwa nini unaoa/kuolewa?
2. Una uhakika uko tayari kwa ndoa?(sio harusi)?
3 Matarajio yako ni nini katika ndoa?
4 Mahitaji yako ni nini katika ndoa?
5. Ni sababu zipi zinaweza kukufanya uachane na mwenzio?
6. Vitu gani usivyopenda kutoka kwake?
7. Vitu gani unapenda kutoka kwake?

Lakini pia muulize mpendwa wako maswali yafuatayo

  • Unapenda tuwe na watoto wangapi (Mungu akitujalia)
  • Mungu asipotujalia mototo katika ndoa yetu utachukua hatua gani?
  • Una maoni gani juu ya njia mbalimbali za uzazi wa mpango?
  • Kama mimi nikipata kazi mbali na wewe unapofanya kazi tutaishije?
  • Dini/dhehebu ikiwa tofauti na wewe tutafanyeje?
  • Una malengo gani katika maisha yako?
  • Unafikiri nini kuhusu talaka?
Hayani maswli machache tu, lakini kupitia haya yataibuka maswali mengine mengi. Mwenzako anapokuuliza haya maswali usifikiri hana upendo kwako au yuko"too judgementa". Lengo lake ni kujua ataishi na mtu wa namna gani na hivyo ajiandae vipi. Maswali haya yanaweza kuibua mawazo na hisia tofauti kati ya wapendanao, na yanapoibuka mawazo na hisia za wawili hawa ndipo wanapozidi kujuana na kuziona tofauti zao za kimtazamo juu ya mambo fulaani. Hii itawasaidia wao kujipanga kukabiliana na tofauti zilizo ibuka wakati wa majadiliano.
Nawashauri vijana wenzangu wasioe au kuolewa kwa sababu tu wanataka kuoa au kuolewa. Ni muhimu wakawa na maandalizi katika akili yao (pre-marital mental preparation).

No comments

Theme images by sbayram. Powered by Blogger.