MH17 yapatikana Maleysia
Wachunguzi wa Kijerumani dhidi ya ndege ya
abiria ya Malaysia ambayo ilipata ajali huko Ukraine mwezi July na
kuripuka angani wanaeleza kua ndege hiyo baada ya kukumbwa na kitu
chenye ncha na kugongwa mara kadhaa na vifaa vyenye mionzi mikali ndio
chanzo cha ajali.Wataalam hao wameendelea kueleza kwamba kisanduku cha kurikodia mwenendo wa ndege hiyo hakikuonesha kwamba kulikua na dharura.
Abiria wote miambili na tisini na nane walipoteza uhai pindi ilipo anza safari kutoka uwanja wa ndege wa Amsterdam kueleke Kuala Lumpur.kutokana na ajali hiyo kuna shaka kwamba vikundi vya waasi wa Urusi viliiidungua ndege hiyo.Lakini mpaka sasa Urusi imepinga kuhusika kwa namna yoyote na ajali hiyo.
Inaarifiwa kwamba ripoti kamili juu ya ndege hiyo MH17 inaweza kupatikana pindi mwakani.
Leave a Comment