NI MAKOSA KUAMINI KUWA NJIA ZA KUMFURAHISHA MWANAMKE AU MWANAUME KATIKA MAHUSIANO NA HASA TENDO LA NDOA ZINAFANANA.
Ni
ukweli usiyopingika kuwa maisha ya leo ni tofauti na ya jana na siku ya
leo ni tofauti na kesho, hii inadhirihika katika mahusiano ya leo.
Watu
wengi wanaoingia katika mahusiano wanashindwa kuajua kuwa kila jambo
lina wakati wake, kuna wakati wa kufurahi na wakati wa huzuni ila kila
wakati una faida yake katika maisha.
Unapokuwa
kwenye mahusiano lazima uwe na wakati wa kujua vema mweza wako ili ujue
nini utafanya ili kumfurahisha pale anapokuwa katika huzuni.
Hali
hii inakufanya uzidi kuwa mwanafunzi na upende somo la mahusiano ya
kimapenzi kwa kuwa somo hili halina mkubwa wala mdogo, wote wanahitaji
kujifunza kwa undani kadri siku zinavyokwenda.
Utakubaliana
na mimi kuwa wanandoa wengi wanadhani kuwa tendo la ndoa au faragha
inafumo maalumu, na ndiyo maana wengine hutwanga na kupepeta na wengine
huona kama ukimshikashika mwanamke inatosha kumbe bado elimu ya ziada
ina hitajika ili kufaulu somo hili lisilokuwa na ukomo katika kulisoma.
Mimi binafsi naamini kuwa maisha yanahitaji umakini mkubwa ili kufanikiwa, pamoja na jitihada na kumwomba Mungu atuwezeshe kufika kule tunakotaka kwenda.
Ndivyo
ilivyo katika mahusiano ni kosa la jinai kuona unajua kila kitu na
kumbe hujui, jifanye ujui ili ujue, na onyesha kiu ya kutaka kujua ili
ujulishwe, kusoma vitabu mbalimbali na kutembelea mitandao mbalimbali ya
jamii.
Jitahidi
hata kama umedumu katika mahusiano kwa miaka mingi tumia muda wako,
kubuni mbinu mpya za mahusiano ili kumfurahisha mume wako au mke wako
kudumisha amani katika mahusiano ni jambo la msingi.
Kuingia
kwenye ndoa au mahusiano si kazi kazi ni kudumu katika mahusiano hayo,
ila yote yanawezekana Endapo utamshirikisha Mungu nyakati zote bila
kuchoka.
Na
hii haijalisho ni mwanamke au mwanaume mnapaswa kushirikiana ili
kubosresha ndoa yenu, kwa kuwa wabunifu na kujituma hata kama umechoka
ndiyo siri ya mafanikio na kuendelea kufatilia www.brunokimaro.blogspot.com kwa
Mahusiano Imara na salama.
Epuka kufanya mapenzi kwa kukariri kuwa huyu anapenda romance kumbe mwezio hapendi, au unamtania mwenza wako kumbe hapendi ila unafanya kwa mazoea epuka hilo.
Kwa kukubali kuwa wewe ni mwanafunzi siku zote uko darasani utajifunza mambo mapya.
Leave a Comment