Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka
nchi TFF, imemfungia wakili Damas Ndumbaro kujihusisha na mambo ya soka
kwa muda wa miaka saba na faini ya kiasi cha pesa. Ndumbaro ambaye aliingia katika mzozo
mkubwa na rais wa TFF, Ndugu, Jamal Malinzi wiki iliyopita baada ya TFF
kuagiza kila klabu kukatwa asilimia tano za mapato yatokanayo na
udhamini wa klabu hizo wanaoupata kutoka kwa Vodacom, wadhamini wakuu wa
ligi kuu ya Tanzania Bara, na Azam Tv.
Ndumbaro alikimbilia katika
vyombo vya habari na kusema wazi kuwa, klabu zimemuagiza kuwaambia TFF
kuwa havipo tayari na havitakubali jambo hilo litokee, huku akijiamini
na kuchambua baadhi ya vipengele na mambo ya sheria, Ndumbaro alivuka
mipaka pale aliposema kuwa wanatafuta wastani wa wajumbe wa mkutano mkuu
wa TFF na kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais wa Shirikisho,
Malinzi.
Kikao cha juzi cha kamati ya nidhamu kimefikia uamuzi wa kumfungia, Ndumbaro na kumlilipisha faini kwa sababu.
Ndumbaro ambaye alizungumza kama wakili
wa klabu za ligi kuu kupitia, Bodi ya Ligi amekanwa ‘ hadharani’ na
vilabu huku vikisema kuwa ‘ havikumtuma’ kuzungumza yale ambayo alisema
mbele ya vyombo vya habari. Klabu zimesema alizungumza kwa ‘ utashi’
wake mwenyewe, na si wao walimtuma.
‘ Kilichomuhuku’ ni yeye kutaka
kubadilisha maamuzi ya kamati ya utendaji ya TFF bila kuthibitishwa na
wajumbe wa Bodi ya Ligi na kukubaliana.
Kupingana maamuzi ya kamati ya utendaji
ni kosa la kinidhamu. Ndumbaro amehukumiwa kutokana na makosa hayo na
kama angezungumza kwa niaba ya klabu basi adhabu hiyo ingekwenda kwa
kwao, lakini yeye alijizungumzia tu
Leave a Comment