MAMBO MAKUBWA YATAKAYO HARIBU MAISHA YAKO
1. Kujiweka wa mwisho na Kujinyima muda wa kufurahi /kustarehe
Maisha yako yamejengwa kwa vipande vidogo vidogo ambavyo kila kimoja kina nafasi yake, na kikikosekana, basi vingine havitakaa kwenye nafasi zake na kuharibu maisha yote.
Wengi tumekuwa tunawapa nafasi wengine kwanza na kuamua kujiweka sisi wa mwisho. Matokeo yake, unajinyima muda wa kupumzika, kula, kustarehe nk! Matokeo yake huwi na furaha na maisha yako!
2.Kukubali kuendeshwa na matukio mabaya yaliyopita
Kuhisi kwa kuwa kuna kitu Fulani kibaya kilikutokea kwenye maisha yako basi
maishahayatawezekana tena. Pengine ulifiwa, kufukuzwa kazi, shule, kuibiwa au kufilisika.
3.Kukubali kuzungukwa na watu wasiokufaa
Ni rahisi, Siku zote watu waliokubali kushindwa, huwa na sababu za kukupa kwa nini wameshindwa kimaisha, na ukikaa karibu nao watakupa sababu hizi na kukufanya uamini kwamba huu ndio ukweli, na hutakuwa tayari kupiga hatua zaidi.
4.Kukimbia matatizo na kuogopa kushindwa
Je wajua? Ukikimbia matatizo yako, siku zote yatakimbia pamoja nawe. Usikimbie tatizo, likabili na kuamka haraka kila tunapoanguka. Na epuka Kuhisi kuna mtu mwingine anahusika na furaha yako.
5. Kuharibu Maisha ya Mwingine ili Ufanikiwe
Ukiharibu maisha ya mwingine, unaharibu ya kwako! Unaweza kuita Karma, Gundu, au majina mengine, lakini jua ya kwamba hii hutokea kweli. Pia ni ngumu kukaa na hayo mafanikio Maana hutakuwa na plani ya pili ya mafanikio zaidi ya kudhurumu, kuiba, kuua nk!
6. Kuamini Wewe ni Mifupa na nyama tu!
Hili ni kosa kubwa sana maishani, wengi huamini binadamu n mifupa na nyama tu, hivyo hakuna hata ya kufanya kazi kwa bidii kwa kuwa tu “eti” Mwisho wa siku tutakufa na kuzikwa! Je, Unawaachia nini wanao na kizazi chako? Je kwa nini hasa Mungu alitupa utashi tofauti na Mbuzi na wanyama wengine?
Kumbuka, Tungeamua kuamini kuwa sisi ni Nyama na mifupa tu, kusingekuwa na Magari, Simu, Majengo ya kisasa, na Hata hii dini tuliyonayo tusingeipata.
“do your part, make world a better place”
7.Kulaumu Vitu vinavyotokea na kutokuwa tayari kutafuta suluhisho Pengine kwa kutotaka kufanya maamuzi magumu au kutojua Majukumu yako ni yapi (badilika)
8. Kuamini kila kinachosemwa na “Wataalamu”
Siku hizi kila sekta kuna watu wanaojiita wataalamu (mimi mmoja wapo!) Lakini nasikitika kukuambia kuwa, wengi wa wataalamu hawa, hawako sahihi kwani siku hizi watu wanapata kipato kutokana na kuyaelewa matatizo ya watu na si kujua suluhisho.
Usimuamini mtu eti tu kwa kuwa analielezea kwa uzuri na analielewa tatizo lako bali muamini anayeweza kutoa suluhisho linalokuwa msaada kwa tatizo lako
9. Kuhisi huwezi kwa kuwa kuna mtu anakuambia hivyo
Kuna watu maishani wapo sii tu kwa kukukwamisha wewe, bali pia kumkwamisha kila anayewazunguka. Ukiona hakubaliki kwa jinsi ulivyo, basi jua huko mahali sahihi. Usikubali kuishi kama mtu mwingine kwa kuwa tu unataka kukubalika maishani.
10. Kuona huhitaji chochote cha kusoma Maisha yanachekesha! Kitu kinaweza kuwepo leo, na kesho kisikuwepo. Kama kuna kitu unataka kufanya, fanya sasahivi. Kama ni wazo la muda mrefu, basi anza leo kutekeleza kidogo kidogo. Kila muda una changamoto zake. Hata tajiri mkubwa duniani Bill gates anachangamoto zake kulingana na nafasi aliyonayo.
Leave a Comment