UNAMJUA ULIYENAYE?

Moja kati ya vitu vinavyowafanya vijana wengi washindwe kufurahia maisha yao ya kimahusiano ni hali ya kwenda jino kwa jino na wapenzi wao. Vijana wengi wanajikuta kila siku wakiingia katika matatizo na  wenzi wao kwa sababau hii.
  Anataka ajue kila mpenzi wake anayewasiliana naye,anataka kila safari ya mpenzi wake aifuatilie mpaka mwisho. Katika hali hii ni lazima tu utajikuta ukiingia katika migogoro isiyo na lazima na mpenzi wako.
   Wakati wewe ukiona uko sahihi kwa msemo wa abiria chunga mzigo wako, mwenzako ataona unafanya dunia isiwe mahala huru kwake. Ndiyo, utakuwa unamnyima uhuru wake. Kuwa naye katika mahusiano haina maana kuwa katengana na dunia nzima.
  Nakubali kuwa inafaa awe na udhibiti wa kuwa na wewe. Ajue tofauti ya sasa na zamani, ila pia jua ana marafiki na watu wake wengine wakaribu hivyo ni lazima tu awe na mawasilaino nao. Huko katika shule na kazini ni lazima tu alikuwa na watu muhimu wa kumsaidia katika masuala mbali mbali ya kimaisha, sasa kuwa na wewe isiwe ndiyo mwisho wa urafiki wao. Suala linalotakiwa hapo ni kuachana na wale tu wanaoonekana kama akiwa nao basi mahusiano yenu kuwa imara ni ndoto za mchana. Unamjua mpenzi wako vizuri?
   Usimbilie kujibu,fikiri kwanza.
   Kumjua vizuri mtu uliye naye itakupa fursa ya kuwa na amani na kujikuta ukiwa mwenye furaha zaidi katika maisha yako. Wengi hawawajui wapenzi wao. Kila wanachoambiwa ama kufanyiwa  wao hufanya kuhisi  na kujilazimisha kuamini. Hawana uhakika na wapenzi wao!
  Kila wanachofanyiwa wanahisi kwa sababau hawajui vizuri wapenzi wao, na dhamira zao za  kuwa na wao. Wewe dhamira ya mpenzi wako unaijua?
   Unajua ni kwanini mpenzi wako kaamua kuwa na wewe? Ni kweli kwa sababu anakupenda au ni kwa sababu hakuna aliyemfuata na kumwambia anampenda? Kuwa makini!
    Wapenzi wengi wako katika mahusiano kwa sababu tu hawana mahala pa kwenda. Wengine wapo katika mahusiano kwa kuwa kwao maisha ni magumu hivyo wanatafuta sehemu ya kupatia unafuu wa maisha. Ukiwa na mtu wa aina hiyo ni vyema kumpa msaada tu kisha kumuacha aendelee na hamsini zake, kwa maana katu mtu wa aina hiyo hana furaha ya kimapenzi kuwa na wewe, na siku mambo yake yakiwa poa tu ni lazima atajitoa katika ‘utumwa anaoutumikia kwako’.
   Una hakika unamjua mapenzi wako vizuri? Kweli umesoma macho yake nakugundua ‘I love you’ yake inamaaisha kile kilichopo katika moyo wake? Mjue mpenzi wako ili uwe na uhakika wa ahadi zenu mnazopanga pamoja.
    Wengine wanapanga ahadi za kuishi milele na wapenzi wao kumbe wenzao wanawatumia kama madaraja ya katika shida zao. Kwani we hujawahi kusikia wakina f’lani wakisomesha alafu baadaye wakakimbiwa? Kwa ni hujawahi kuona wanapendwa katika kipindi cha raha wakipata matatizo wanakimbiwa? Hujawahi kuona? Mwenzio nimewahi!
   Na yote hii inasabababishwa kwa kutowajua vizuri wapenzi wao. Unafikiri kama ukimjua vizuri mpenzi wako yote yatakutokea? Wapi!
    Wakati yeye akijua yuko na zoba wa kupita, wewe unamuona mjinga kwa kutojua kama umemjua. Wanaonung’unika leo na kulia yasingewakuta hayo kama wangewajua wapenzi wao mapema. Wala usidhani kuwa ni tabu. Si hivyo!
   Anza kuwa makini na matendo ya mwenzako kuanzia sasa. Acha kuchunguza katika namna isiyofaa. Mpe uhuru unaostahili alafu kuwa makini na maneno na matendo yake kwako. Pia zingatia sana mahitaji yake kwako. Je,yanalengo la kukomoa au kuna kitu kingine?
  Wengi kutokana na mapenzi yao kwa wenzao wamejikuta wakijitahidi kuwawatimizia mahitaji wanayoyataka wakidhani ni njia ya kuonesha mapenzi yao kumbe wenzao wanawachukulia tofauti. Wanaowaona wajinga wasiojua wanalofanya. Kuwa makini sana na mwenzako unaweza kumchukulia tofauti bure. Unaweza kudhani si anayekufaa kumbe akawa ndiye mwenye uwezo wa kukufuta machozi, au vinginevyo.

No comments

Theme images by sbayram. Powered by Blogger.