Faida
ipi hiyo zaidi ya maumivu na mateso ya moyo? Jamani ni kweli kabisa
kwamba kuna maumivu na karaha nyingi unaponuniana na mpenzi wako, lakini
wakati huo huo kuna faida nyingi za kununiana naye. Mapenzi yana wigo
mpana mno ambao mtu anapaswa kuuangalia kwa jicho pana na akili pembuzi
kabla ya kuingia,namaanisha kwamba ni lazima kuchunguza kina cha maji
kabla ya kuzamia. Sasa basi, zifuatazo ni faida tano utakazozipata
ukiwa umenuniana na mpenzi wako.
HUSAIDIA KUPUNGUZA MIGOGORO
Ni
ukweli usiopingika kuwa, katika hali ya kawaida, ukiwa mbali na mtu
fulani katika jamii unayoishi ni vigumu sanakujikuta umekwaruzana naye.
Hii ni kwasababu utakuwa hauingiliani nayekatika mizunguko yako, vivyo
hivyo kwa wapenzi walionuniana.Hali hii hupunguza kabisamigogoro ya
hapa na pale, kwani hiki ni kipindi ambacho mtakuwa mbalimbali jambo
ambalo huepusha maudhi ya kibinadamu.Mfano, yawezakana katika kipindi
mlichonuniana na mpenziwako, uliingia ujumbe wa mapenzi kwenye simu yake
kutoka kwa mtu aliyekosea namba. Kwa kuwa hauko naye karibu jambo hili
halitakuumiza maana hutaelewa nini kimeendelea tofauti na kama
ungelikuwa naye karibu.Kwa hiyo kuna baadhi ya maumivu na maudhi ambayo
utaepukana nayokwa kipindi cha kununiana kwenu. Ni kweli kabisa kwamba
hupunguza migogoro na mitafaruku ya hapa na pale, umeelewa mpenzi
msomaji wangu? Haya twende kwenye faida ya pili.
KUBAINI TABIA X ZA MWENZAKO
Hiki
ni kipindi ambacho sasa kitakusaidia wewe kubaini tabia na mienendo
mibaya ya mwenzi wako. Hii ni kwa kuwa utakuwa mbali naye hivyo naye
hujiona kuwa yuko huru kufanya jambo lolote analoona kuwa linafaa bila
kujali uwepo wako kwani kila mtu ana ‘time’ na mwenzake.Kama kuna asili
ya maisha yake ambayo aliiacha baada ya kuingia katika uhusiano na
wewe,ambayo ni mbaya zaidi sasa hapa ataanza kuirudia kwa kujiona kuwa
hana mtu wa kumzuia na kumbana.Kama ni mlevi kupindukia,mchafu, muongo
na tabia nyingine mbaya za kufanana na hizi basi ataanza kuzionesha
katika kipindi ambacho mmenuniana.
KUPATA MUDA WA KUTAFAKARI ZAIDI
Hapa
naomba nieleweke vizuri kabisa kwamba, ninapoongelea suala la
kutafakari zaidi katika kipindi ambacho wewe hauna maelewano mazurina
mwenzi wako, namaanisha kuwa utapata muda mzuri zaidi wa kutafakari
penzi lenu kwa ujumla.Ni kipindi kitachokuongoza wewe kuwa na uelewa wa
ni aina gani ya mpenzi uliyenaye. Kivipi? Ni kwamba, katika muda huu
mara nyingi utataka kupata suluhu ya kununiana kwenu, lakini pia katika
kutafuta suluhuhiyo utapata fursa ya kutafakari kwa kina juu yapenzi
lenu huku ukimpima mwezi wako kwa mtazamo chanya.
KUFAHAMU AINA YA MARAFIKI ZAKE
Si
kila rafiki wa mwenza wako ana nia nzuri na uhusiano wenu au
anafurahia penzi lenu. Mathalani, labda wewe ni msichana na pengine
miongoni mwa rafiki zakekuna mmoja au wawili ambao hutamani sana kupata
penzi lako.Sasa katika kipindi ambacho utakuwa umenuniana na mpenzi
wako basi itakuwa ni nafasi nzuri kwao kuitumia kunyunyizia sumu ya
kumponda huku wakikutamkia maneno ya kukushawishi, hivyo utakuwa
umeelewa ni aina gani ya marafiki alionao mwenzi wako.Hii si kwa
msichana tu, hata kwa wanamume kwani huenda kati ya rafiki wa
‘girlfriend’ wako, kuna wanaokutamani, sasa wakiona huna uhusiano mzuri
na mpenzi wako, watatumia nafasi hii kukuambia maneno ya uongo juu
yake na kukuonesha kila dalili za kukutaka.Hivyo utakuwa umefahamu ni
aina gani ya rafiki ambao mpenzi wako anao. Tambua kwamba, marafiki
wengi wana tabia zinazofanana.
KUBAINI AINA YA PENZI ALILONALO KWAKO
Katika
kipindi hiki, utaweza kuelewa ni aina gani ya penzi alilonalo huyo mtu
wako juu yako. Kwa mpenzi aliye na hisiaza dhati kabisa kwako, katika
kipindi hiki atakuwa ni mtu wa kutafuta njia ya kupata suluhu ya tatizo
lenu.Pamoja na kwamba wewe utakuwa umenuna, bado yeye ataonesha
kukujali kama kawaida, atakupigia simu za hapa na pale yaani ilimradi
tu asikie angalau sauti yako,lengo lake likiwa ni kutaka kurejesha
ukaribu ambao sasa anaona kama akiupoteza itakuwa ni maumivu kwake.Kwa
mantiki hiyo basi, utagundua ni kwa jinsi gani anathamini penzi lenu na
ni aina gani ya penzi alilonalo kwako. Yote haya utabahatika kuyajua
kupitia kipindi cha kununiana kwenu.Hata hivyo, niwatahadharishe
kwamba, kuandika haya isiwe ni tiketi ya wewe sasa kuanza kununiana na
mpenzi wako eti kwa kigezo kwamba utapata nafasi ya kumfahamu, la
hasha! Siku zote katika uhusianowako epuka maudhi na migogoro isiyokuwa
ya maana.
Leave a Comment