ANA UJAUZITO WAKO? MSAIDIE KWA KUFANYA HAYA
Uhali gani mpendwa msomaji wangu, ni matumaini yangu kwamba uko poa
na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku. Karibu tena kwenye
uwanja wetu huu tujadiliane na kuelekezana kuhusu mambo mbalimbali
yahusuyo uhusiano wa kimapenzi.
Sote
tunaelewa kwamba hakuna kipindi kigumu katika uhusiano wa kimapenzi
kama pale mwenzi wako anaponasa ujauzito. Wanawake wengi huwa na
mabadiliko makubwa ya tabia, hali inayowafanya wanaume wengi washindwe
kujua namna ya kuishi nao katika kipindi hicho kigumu.
Unampenda na unataka kumuonesha jinsi unavyomjali lakini mwenyewe hata haelekei. Kila unachokifanya anakiona kibaya, kila kitu kinamkasirisha, muda wote anakuwa na hasira au kisirani kiasi cha kufanya uione nyumba yako kuwa chungu? Usijali, unapaswa kumuelewa na kumsaidia kwani anakuwa katika kipindi kigumu sana kihisia, kiakili na kimwili.
MFANO HALISI
Jackson, mkazi wa Morogoro alifunga ndoa na mkewe kipenzi miezi michache iliyopita. Tayari mkewe huyo ameshanasa ujauzito lakini mabadiliko makubwa ya tabia zake, yanamfanya Jackson ahisi kwamba huenda mkewe amepata mwanaume mwingine au hampendi tena.
“Kabla hajapata ujauzito, tulikuwa tukielewana na kupendana sana lakini tangu apate tu ujauzito, nyumba naiona chungu. “Ananikaripia kama mtoto mdogo, kila ninachofanya anaona nakosea.
“Anaweza kuniagiza nimletee zawadi kwa mfano matunda lakini jioni nikimpelekea, atayatoa kasoro kuanzia mwanzo mpaka mwisho kisha anaenda kuyatupa, hivi ni haki kweli hii? Kwenye tendo la ndoa ndiyo kabisa hataki hata nimguse.
“Muda mwingine ananiambia nanuka jasho hata kama nimetoka kuoga muda huohuo.
Naomba ushauri hivi ananipenda kweli huyu?”Bila shaka msomaji wangu umemuelewa vizuri Jackson anachokisema.Kinachomtokea ndugu yetu huyu, ndicho kinachowatokea wanaume wengi, hasa ambao wake zao au wenzi wao wamepata ujauzito wa kwanza.
NINI CHA KUFANYA?
Hakuna kipindi ambacho mwanaume anapaswa kumnyenyekea mwenzi wake, kumjali na kumuonea huruma kama kipindi ambacho ameshika ujauzito. Safari ya miezi tisa kubeba kiumbe tumboni si mchezo, wanawake wenyewe watakuwa mashahidi kwa jinsi safari ya kulea ujauzito mpaka kujifungua ilivyo ngumu.
Katika kipindi hiki, ni kawaida kabisa kwa mwanamke kuonesha mabadiliko makubwa kama nilivyosema hapo awali, hasa kipindi ambacho mimba inakuwa bado changa. Ni kipindi ambacho anaweza kusema au kufanya jambo lolote bila kujali madhara yake.
Anakuwa siyo yeye tena, tayari amebeba mzigo mzito ambaye mtu pekee wa kumfariji ni wewe. Wapo baadhi ya wanawake wakibeba ujauzito, huwachukia sana waume zao lakini hali hiyo huisha mara tu baada ya kujifungua au ujauzito kuwa mkubwa.
Haina maana kwamba mapenzi yameisha ndiyo maana hakupendi, la hasha. Anakuwa anakupenda sana lakini hali yake ndiyo inayomsababishia awe hivyo. Huna haja ya kukasirika hata kama atakuwa anakuudhi na kukukasirisha kiasi gani.
Zipo mbinu nyingi za namna ya kuishi na mwenzi wako akiwa katika hali hii bila kusababisha migogoro ya aina yoyote.
Nakushukuru wewe msomaji wangu ambaye ulishiriki kutuma ujumbe wako na kutoa ushauri kwa msomaji Jackson wa Morogoro ambaye alikuwa akilalamika jinsi mkewe alivyobadilika tabia baada ya kubeba ujauzito kiasi cha kuwa anamkasirisha mara kwa mara.
NI HALI YA KAWAIDA
Wasomaji wangu wengi, hasa ambao tayari wanao uzoefu wa mabadiliko yanayotokea katika kipindi cha ujauzito, wamesema kwamba ni jambo la kawaida kabisa kwa mwanamke kubadilika kitabia na kihisia baada ya kunasa ujauzito.
“Mimi mwenyewe wakati nikiwa mjamzito, nilikuwa namchukia sana mume wangu kiasi cha kuwa nalala sebuleni kila siku ili kukwepa kulala naye. Nilikuwa naona ananikera kila kitu anachokifanya lakini namshukuru mume wangu alinielewa. Nilipojifungua, kile kisirani kimeisha kabisa na tunapendana sana,” alichangia msomaji wangu, Mama Kelvin wa Tabata.
Jambo muhimu la kujifunza, ni kwamba mwenzi wako anapobadilika tabia kwa sababu ya ujauzito, elewa kwamba hiyo ni hali ya kawaida kabisa na itaisha baada ya muda mfupi, cha msingi ni kumvumilia na kuendelea kumuonesha mapenzi ya dhati.
NAMNA YA KUISHI NA MWENZI MJAMZITO
Hakuna kipindi ambacho mwanamke anahitaji kuoneshwa kwamba unampenda, unamjali na unafurahia yeye kuwa na mzigo wako kama kipindi ambacho anakuwa na ujauzito.
Jambo ambalo watu wengi hawalijui, baada ya ujauzito kufikia kipindi fulani, mtoto anayekuwa tumboni anachangia vitu vingi sana na mama yake. Mama anapokasirika, anazalisha kemikali/homoni ambazo zinaenda kumuathiri mtoto moja kwa moja tumboni.
Hali kadhalika, mama akiwa anafurahi mara kwa mara, mtoto aliyepo tumboni naye anafurahi na hata ukuaji wake unakuwa mzuri. Hata kama hukuwa na mazoea ya kuwa karibu na mwenzi wako awali, jifunze kuwa karibu naye, kumbembeleza, kupiga naye stori za kufurahisha na kumueleza jinsi unavyofurahi kuelekea kuitwa baba wa mtoto aliye ndani ya tumbo lake.
Mbusu tumbo lake mara kwa mara, msikilize mtoto anavyocheza na msaidie kufanya mazoezi mepesi ikiwa ni pamoja na kutembea pamoja jioni, kuhakikisha anapata chakula bora na matumizi mengine muhimu na kubwa zaidi muandalie mazingira salama ya kujifungulia.
Hivi ni vitu ambavyo vitamjenga sana mwenzi wako kisaikolojia na hakika vitamsaidia hata kuja kujifungua salama.
Epuka kumkaripia, kumuudhi au kumpiga mwenzi wako akiwa mjamzito.
Msamehe kwa kila anachokosea, jirekebishe kwa kila kinachomuudhi na mara zote muonee huruma kwani kuna kazi kubwa inakuja mbele yake, ya kukuletea mtoto duniani.
Ukifanya hivyo, hakika utakuwa mwanaume bora na baba bora wa familia.
Sote
tunaelewa kwamba hakuna kipindi kigumu katika uhusiano wa kimapenzi
kama pale mwenzi wako anaponasa ujauzito. Wanawake wengi huwa na
mabadiliko makubwa ya tabia, hali inayowafanya wanaume wengi washindwe
kujua namna ya kuishi nao katika kipindi hicho kigumu.Unampenda na unataka kumuonesha jinsi unavyomjali lakini mwenyewe hata haelekei. Kila unachokifanya anakiona kibaya, kila kitu kinamkasirisha, muda wote anakuwa na hasira au kisirani kiasi cha kufanya uione nyumba yako kuwa chungu? Usijali, unapaswa kumuelewa na kumsaidia kwani anakuwa katika kipindi kigumu sana kihisia, kiakili na kimwili.
MFANO HALISI
Jackson, mkazi wa Morogoro alifunga ndoa na mkewe kipenzi miezi michache iliyopita. Tayari mkewe huyo ameshanasa ujauzito lakini mabadiliko makubwa ya tabia zake, yanamfanya Jackson ahisi kwamba huenda mkewe amepata mwanaume mwingine au hampendi tena.
“Kabla hajapata ujauzito, tulikuwa tukielewana na kupendana sana lakini tangu apate tu ujauzito, nyumba naiona chungu. “Ananikaripia kama mtoto mdogo, kila ninachofanya anaona nakosea.
“Anaweza kuniagiza nimletee zawadi kwa mfano matunda lakini jioni nikimpelekea, atayatoa kasoro kuanzia mwanzo mpaka mwisho kisha anaenda kuyatupa, hivi ni haki kweli hii? Kwenye tendo la ndoa ndiyo kabisa hataki hata nimguse.
“Muda mwingine ananiambia nanuka jasho hata kama nimetoka kuoga muda huohuo.
Naomba ushauri hivi ananipenda kweli huyu?”Bila shaka msomaji wangu umemuelewa vizuri Jackson anachokisema.Kinachomtokea ndugu yetu huyu, ndicho kinachowatokea wanaume wengi, hasa ambao wake zao au wenzi wao wamepata ujauzito wa kwanza.
NINI CHA KUFANYA?Hakuna kipindi ambacho mwanaume anapaswa kumnyenyekea mwenzi wake, kumjali na kumuonea huruma kama kipindi ambacho ameshika ujauzito. Safari ya miezi tisa kubeba kiumbe tumboni si mchezo, wanawake wenyewe watakuwa mashahidi kwa jinsi safari ya kulea ujauzito mpaka kujifungua ilivyo ngumu.
Katika kipindi hiki, ni kawaida kabisa kwa mwanamke kuonesha mabadiliko makubwa kama nilivyosema hapo awali, hasa kipindi ambacho mimba inakuwa bado changa. Ni kipindi ambacho anaweza kusema au kufanya jambo lolote bila kujali madhara yake.
Anakuwa siyo yeye tena, tayari amebeba mzigo mzito ambaye mtu pekee wa kumfariji ni wewe. Wapo baadhi ya wanawake wakibeba ujauzito, huwachukia sana waume zao lakini hali hiyo huisha mara tu baada ya kujifungua au ujauzito kuwa mkubwa.
Haina maana kwamba mapenzi yameisha ndiyo maana hakupendi, la hasha. Anakuwa anakupenda sana lakini hali yake ndiyo inayomsababishia awe hivyo. Huna haja ya kukasirika hata kama atakuwa anakuudhi na kukukasirisha kiasi gani.
Zipo mbinu nyingi za namna ya kuishi na mwenzi wako akiwa katika hali hii bila kusababisha migogoro ya aina yoyote.
Nakushukuru wewe msomaji wangu ambaye ulishiriki kutuma ujumbe wako na kutoa ushauri kwa msomaji Jackson wa Morogoro ambaye alikuwa akilalamika jinsi mkewe alivyobadilika tabia baada ya kubeba ujauzito kiasi cha kuwa anamkasirisha mara kwa mara.
NI HALI YA KAWAIDA
Wasomaji wangu wengi, hasa ambao tayari wanao uzoefu wa mabadiliko yanayotokea katika kipindi cha ujauzito, wamesema kwamba ni jambo la kawaida kabisa kwa mwanamke kubadilika kitabia na kihisia baada ya kunasa ujauzito.
“Mimi mwenyewe wakati nikiwa mjamzito, nilikuwa namchukia sana mume wangu kiasi cha kuwa nalala sebuleni kila siku ili kukwepa kulala naye. Nilikuwa naona ananikera kila kitu anachokifanya lakini namshukuru mume wangu alinielewa. Nilipojifungua, kile kisirani kimeisha kabisa na tunapendana sana,” alichangia msomaji wangu, Mama Kelvin wa Tabata.
Jambo muhimu la kujifunza, ni kwamba mwenzi wako anapobadilika tabia kwa sababu ya ujauzito, elewa kwamba hiyo ni hali ya kawaida kabisa na itaisha baada ya muda mfupi, cha msingi ni kumvumilia na kuendelea kumuonesha mapenzi ya dhati.
NAMNA YA KUISHI NA MWENZI MJAMZITO
Hakuna kipindi ambacho mwanamke anahitaji kuoneshwa kwamba unampenda, unamjali na unafurahia yeye kuwa na mzigo wako kama kipindi ambacho anakuwa na ujauzito.
Jambo ambalo watu wengi hawalijui, baada ya ujauzito kufikia kipindi fulani, mtoto anayekuwa tumboni anachangia vitu vingi sana na mama yake. Mama anapokasirika, anazalisha kemikali/homoni ambazo zinaenda kumuathiri mtoto moja kwa moja tumboni.
Hali kadhalika, mama akiwa anafurahi mara kwa mara, mtoto aliyepo tumboni naye anafurahi na hata ukuaji wake unakuwa mzuri. Hata kama hukuwa na mazoea ya kuwa karibu na mwenzi wako awali, jifunze kuwa karibu naye, kumbembeleza, kupiga naye stori za kufurahisha na kumueleza jinsi unavyofurahi kuelekea kuitwa baba wa mtoto aliye ndani ya tumbo lake.
Mbusu tumbo lake mara kwa mara, msikilize mtoto anavyocheza na msaidie kufanya mazoezi mepesi ikiwa ni pamoja na kutembea pamoja jioni, kuhakikisha anapata chakula bora na matumizi mengine muhimu na kubwa zaidi muandalie mazingira salama ya kujifungulia.
Hivi ni vitu ambavyo vitamjenga sana mwenzi wako kisaikolojia na hakika vitamsaidia hata kuja kujifungua salama.
Epuka kumkaripia, kumuudhi au kumpiga mwenzi wako akiwa mjamzito.
Msamehe kwa kila anachokosea, jirekebishe kwa kila kinachomuudhi na mara zote muonee huruma kwani kuna kazi kubwa inakuja mbele yake, ya kukuletea mtoto duniani.
Ukifanya hivyo, hakika utakuwa mwanaume bora na baba bora wa familia.
Nitafute facebook Mr Clever Blog
Twitter @Mr Clever Blog
Instagram Mr_Clever_Blog
Leave a Comment