MBUNGE WA MVOMERO AINGILIA KATI MGOGORO WA BONDE LA MGONGOLA
Mbunge wa Mvomero, Mh Amos Makalla akiongea na wananchi nje ya kituo cha polisi kuwa mahabusu wapo salama
Mbunge
wa Mvomero, mkuu wa wilaya , Kamati ya ulinzi na usalama na wenyeviti
wa Vijiji wakiwa kituo cha polisi Dakawa kuwaona mahabusu wanaoshikiliwa
polisi kufuatia machafuko ya wakulima na wafugaji watu 3 wamekufa.
Mbunge
wa Mvomero Mh, Amos Makalla ameridhia pendekezo la wananchi kumuona
Waziri Mkuu Mh, Mizengo Pinda kufuatia mapigano ya wakulima na wafugaji
yaliyotokea wiki iliyopita ambapo watu watatu walipoteza maisha huku
wengine wengi wakijeruhiwa baada ya wafugaji kulishia Mazao ya wakulima
katika mashamba yaliopo bonde la mgongola.
Kutokana
na hali hiyo, Mbunge huyo kwa kushirikiana na Mkuu wa wilaya na kamati
ya ulinzi na usalama waliitisha mkutano wa hadhara kijiji cha Kugugu
kuongea na wakulima wanaolima katika bonde la Mgongola, ambapo pamoja na
mambo mengine wananchi walimuomba Mbunge wao kuundwe Kamati ya kumuona
Waziri mkuu Mizengo Pinda kuhusiana na mipaka ya bonde la Mgongola
ambalo limekuwa mahakamani kwa zaidi ya miaka 15 na machafuko ya mara
kwa mara yametokana na bonde hili kwa wafugaji wa kijiji cha Kambala
kulishia mifugo Mazao ya wakulima na kupelekea uvunjifu wa Amani wa mara
kwa mara.
Akiongea
kwa niaba ya wananchi, mkazi wa Kigugu ndugu Salihina Mpenda alisema
kuwa "kesi ya bonde la Mngongola imekuwa muda mrefu na serikali
haichukui hatua huku watu wanaendelea kufa kila kukicha, na imefika
wakati jitihada zako Mbunge ulizozifanya kuwaleta mawaziri 4, barua
ulizomuandikia Waziri mkuu na Waziri wa ardhi sisi wananchi
tunakupongeza ila inapaswa tukuongezee nguvu tukamuone Waziri mkuu"
alisema mkulima huyo.
Akijibu
hoja hiyo, Mbunge na Naibu Waziri aliridhia ombi lao la kuundwa Kamati
ya wakulima ya kumuona Waziri mkuu na akawataka wachague watu kumi na
yeye kama Mbunge atagharamia gharama zote.
Aidha
kwa upande mwingine mkuu wa wilaya hiyo Festo Kiswaga amewahakikishia
hali ya usalama ndani ya bonde la Mgongola ni shwari wakulima waendelee
na shughuli zao kwani na Ulinzi wa Askari wa doria umeimarishwa.
Leave a Comment