Uandikishaji Wanachama ‘Tanzania Bloggers Network’ (TBN)
Chama
cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini ‘Tanzania Bloggers
Network’ – TBN kinapenda kuwajulisha wanaotaka kujiunga na chama hicho
kuwa fomu za kujiunga zinatolewa. Wahusika ni wamiliki na waendeshaji
wote wa mitandao ya kijamii (blogs na forums) Tanzania na Watanzania
wanaofanya kazi kama hiyo nje ya nchi.
Sifa kuu kwa mwanachama ni kuwa na
blog ambayo ina umri wa miezi sita tangu ianze kuendeshwa mfululizo.
Kwa wa kazi wa Dar es Salaam wenye sifa ambao wanataka kujiunga fomu
hizo zinapatikana kwenye Ofisi za Muda za Tanzania Bloggers Network
(TBN) kwenye Jengo la Dar Free Market lililopo mkabala na Barabara ya
Ally Hassan Mwinyi.
Mwanachama muitaji wa kujiunga
kabla ya fomu atatakiwa kutoa shs 25,000/- ikiwa ni Kiingilio cha
mwanachama, shs 15,000/- yakiwa ni malipo ya ada ya miezi mitatu kwa
mwanachama na shs 10,000/- ikiwa ni malipo ya kadi ya TBN kwa mwanachama
(utambulisho). Jumla kuu kila mwanachama anatakiwa kulipa shs 50,000/-
na kupewa risiti halali ya malipo ya TBN. Fomu zitatolewa siku za kazi
kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni. Zoezi la utoaji fomu
litasimamiwa na Mweka Hazina wa TBN, Shamim Mwasha (0767418941). Fomu
pia zinapatikana Ofisi za Michuzi Media, mjini Jengo refu karibu na
Hospitali ya Ocean Road ghorofa ya pili.
Kwa wanachama wa mikoani utaratibu
unafanywa namna ya kusambaza fomu hizo mara moja na wanachama watalipa
moja kwa moja benki ya NMB kwenye akaunti ya TBN. Utaratibu unafanywa
kupata viongozi wa kanda wa muda watakaoratibu usajili kwa kushirikiana
na viongozi wa muda wa TBN taifa. Viongozi wa muda wa mikoa na kanda
watapewa maelekezo namna ya kusimamia na kuratibu zoezi la kujiunga
uwanachama wa TBN.
Mikoani TBN itagawanyika kwa
kanda, yaani Kanda ya Pwani (ikijumuisha mikoa ya Tanga na Pwani
yenyewe), Kanda ya Zanzibar (ikijumuisha Unguja na Pemba), Kanda ya Dar
es salaam, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (inayojumuisha mikoa ya Iringa,
Mbeya, Rukwa, Simiyu), Kanda ya Kusini (jumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara
na Ruvuma), Kanda ya Kati (mikoa ya Dodoma, Tabora, Morogoro na
Singida), Kanda ya Magharibi (inayojumuisha mikoa ya Kigoma na Rukwa),
Kanda ya Ziwa (yenye mikoa ya Kagera, Geita, Mara na Mwanza), na Kanda
ya Kaskazini (inayojumisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara).
Kwa wahitaji unaombwa kuchukua
fomu yako mapema kwani usajili wa wanachama wa TBN utafanyika kwa muda
wa wiki tatu kisha zoezi hili litafungwa ili kutoa fursa kwa viongozi na
kamati husika kutathmini wanachama waliopatikana na litafunguliwa tena
baada ya miezi sita.
NB;- Kwa watakaohitaji katiba ya
TBN watapewa pia ofisini coppy, lakini coppy hiyo wataigharamia wenyewe.
Utaratibu unafanywa wa kuichapa kwenye soft coppy na zitatumwa mikoani
kwa gharama za TBN.
Imetolewa na:
Joachim Mushi, 0756469470
Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN)
Joachim Mushi, 0756469470
Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN)

Leave a Comment