HAKUNA MAFUNZO KWA MADEREVA KILA BAADA MIAKA MITATU

Kamanda wa Pol
litakapokamilika kwa mchakato wake. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa
madereva nchini, Clement Masanja. isi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, DCP Mohammed
R. Mpinga – DCP (kulia) akitoa maelezo ya kiutalaamu juu ya suala la
kusoma kwa madereva ambalo kwa sasa suala hilo limesitishwa hadi hapo. Taarifa hiyo aliitoa jijini
katika ukumbi wa habari MAELEZO, jijini Dar es Salaam.
TAARIFA KWA UMMA
Hivi
karibuni nchi yetu imekumbwa na Migomo ya Madereva iliyopelekea adha
kubwa kwa wananchi pamoja na kuathiri uchumi wa nchi yetu. Mojawapo ya
madai ya madereva ilihusiana na kukataa kwenda kusoma pamoja na gharama
ya mafunzo kudaiwa kuwa Ths 560,000/=.
Ndugu Waandishi wa habari,
Katika
kukabiliana na ajali za Barabarani, Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama
Barabarani kiliona kuna upungufu katika eneo la Ukaguzi wa magari,
muenekeno wa magari makubwa yanapo haribika usiku, ulipaji wa faini ya
papo kwa papo, na elimu duni au umuhimu wa kusoma kwa madereva kila
baada ya kipindi fulani.
Hivyo moja
ya kanuni iliyolalamikiwa sana na madereva na kuwa sababu mojawapo ya
migomo, ni ile inayowataka madereva wa mabasi na malori kwenda kusoma,
kuangaliwa afya kisha kujaribiwa kila baada ya miaka 3 na pia kuwataka
madereva wa magari mengine kuangaliwa afya na kujaribiwa kila baada ya
miaka 6 ( The Road Traffic ( Examination and Re-Testing of Drivers)
Regulation GN No 31 ya 30/01/2015. Mchakato wa kuandaa kanuni hii
ulianza tokea mwanzoni mwa mwaka 2014 na kupitia hatua mbali mbali
ulioshirikisha wadau toka TRA, SUMATRA, NIT, Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, TABOA, TATOA, Vyama vyama vya Madereva n.k.
Ndugu Waadishi wa Habari,
Kimsingi
hitaji la kupata mafunzo ya muda mfupi (refresher course) kila baada ya
miaka 3 lililoko kwenye kanuni hizi linawahusu madereva wenye leseni za
madaraja E, C, C1, C2, na C3 ambapo wanaweza kupata mafunzo hayo muda
wowote kabla leseni haijafikia muda wake wa kuhuishwa. Halikadhalika
kanuni hizi zimeweka hitaji la dereva yeyote anayetaka kupata leseni
daraja E kupata mafunzo ya kuenda magari makubwa na zinampatia mamlaka
Mkuu wa jeshi la Polisi (IGP) kumwamuru dereva yeyote kurudi shule
endapo ataonekena kufanya kitendo hatarishi. Aidha katika kanuni hizi,
hakuna chuo kilichotajwa kutoa mafunzo ya “Refresher” yatakayochukua
siku 3 hadi 5 na wala matayarisho ya mtaala wake hayajakamilika.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Nichukue
nafasi hii kuwajulisha madereva wote wa vyombo vya moto na wananchi kwa
ujumla, Mwaka huu hakutakuwa na mafunzo au kutakiwa kwenda kusoma kwa
mujibu wa mahitaji ya kanuni hizi. Mitaala ya mafunzo haya mafupi
haijakamilika na shule zitakazo husika hazijaanishwa aidha ada za
mafunzo hazijapangwa na ada ya Ths ya 560,000/= haijawahi kutamkwa na
serikali.
Kwa
madereva ambao leseni zao zimekwisha au zitaisha katika kipindi hiki
watabadilishiwa/kuhuisha leseni zao kwa utaratibu wa zamani bila
kuulizwa vyeti vya mafunzo mafupi (Refresher course).
Mwisho
niwatake madereva wote wawe na uvumilivu kwa matatizo na changamoto zao
kwani kamati ya Kudumu ya kutatua matatizo katika sekta ya usafirishaji
iliyoundwa na Mhe. Waziri Mkuu itayapatia ufumbuzi wa kudumu.
Imetolewa:-
Mohammed R. Mpinga – DCP
KAMANDA WA POLISI
KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI ( T )
13th May, 2015
Leave a Comment