Hatimaye mgomo wa mabasi umeisha


Hali ilivyo katika kituo kikuu cha Mabasi Ubungo leo.
Hali ilivyo katika kituo kikuu cha Mabasi Ubungo leo.
Ule mgomo wa mabasi uliodumu kwa muda wa siku mbili hatimaye umeisha baada ya madereva kutangaza kuumaliza mgomo huo ulioanza jana Jumatatu, baada ya kufikia muafaka na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mh. Paul Makonda.
Muafaka huo umefikiwa muda mfupi baada ya kuundwa kwa kamati itakayosimamia matatizo ya madereva hao kwa kutoa taarifa ndani ya siku saba kuhusu malalamiko yao.
Taarifa hiyo imepelekea mabasi yaliyokua katika kituo cha mabasi Ubungo, jijini Dar es Salaam, kuanza safari zake mara moja kuelekea mikoani na yale ya mikoani kuelekea mikoa husika kulingana na safari zao.
Makubaliano yaliyofikiwa ni kuundwa kwa kamati ya madereva zaidi ya 8 watakaokutana na Mkuu wa Wilaya kuanzia kesho Jumatano.
Kamati iliyoundwa inatakiwa kujadili madai ya madereva kwa muda usiozidi siku saba chini ya usimamizi wa Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Mh. Makonda.

No comments

Theme images by sbayram. Powered by Blogger.