MSICHANA ALIYEUA MTOTO WA MIAKA 9,AFIKISHWA MAHAKAMANI,APIGWA NGUMI MBELE YA POLISI MKOANI MOROGORO!

 
Msichana Judith Chomile(15) amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro akikabiliwa na tuhuma za kumnyonga hadi kufa mtoto mwenye umri wa miaka 9 mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Bernard Benderi ya mjini Morogoro.
 
Akisoma shitaka mbele ya hakimu mkazi Ivan Msaki, mwendesha mashataka wa polisi Aminata Mazengo amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo may 20 kinyume na kifungu namba 196 cha kanuni ya adhabu nahakutakiwa kujibu lolote kutokana na kosa lenyewe na kuwa mtuhumiwa yuko chini ya miaka 18 hivyo kuwakilishwa.
 
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 10 mwaka huu itakapo tajwa tena mahakamani hapo .
Katika hali isiyo ya kawaida ndugu wa marehemu Edga Mafwere kwa hasira amempiga ngumi mtuhumiwa muda mfupi baada ya kutoka mahakamani mbele ya maafisa wa jeshi la polisi na ustawi wa jamii ambapo naye alijikuta katika mikono ya jeshi la polisi na kufungwa pingu ambapo anashikiliwa kwa mahojiano zaidi.
 
Akizungumza juu ya uhakika wa usalama wa mschana Judith Chomile ,afisa ustawi wa jamii manispaa ya Morogoro Jasmin Masenge amesema msichana huyo atakuwa katika mikono salama chini ya uangalizi wa kitengo cha ustawi wa jamii pamoja na jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia na watoto hadi kesi inayomkabili itakapotolewa hukumu.

No comments

Theme images by sbayram. Powered by Blogger.