Dk Utaro mwenyekiti mpya JET
Mwenyekiti
mteule wa Chama cha Waandishi wa Habari Mazingira Tanzania (JET),
Dk.Elen Utaro akitoa shukrani zake kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa
uchanguzi wa chama hicho kwa kumpatia kura za kutosha na amewataka wampe
ushirikiano wa kutosha ili kukiendeleza mbele chama hicho.
Kaimu
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Mazingira Tanzania
(JET), Aisha Dachi, akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Chama cha
Waandishi wa Habari Mazingira ambapo alitangza hagombei tena nafasi hiyo
kwa madai anachukia ‘Ukurunzinza’. Kulia ni Katibu Chrysostom Rwemamu
na kushoto ni Katibu mtendaji JET John Chikomo.
Baadhi ya
wajumbe wa mkutano mkuu wa uchanguzi wa Chama cha Waandishi wa Habari wa
Mazingira Tanzania (JET) waliohudhuria mkutano huo uliofanyika kwenye
ukumbi wa mikutano wa Lion Sinza jijini Dar-es-salaam.
Kaimu
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET)
aliyemaliza muda wake, Aisha Dachi, akimkabidhi Frank Kimaro (54) mkazi
wa mkoa wa Kilimanjaro, tuzo na shilingi milioni moja kwa juhudi zake
za kutunza vyanzo vya maji.
Na Nathaniel Limu, Dar es Salaam
MKUTANO
mkuu wa uchanguzi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira
Tanzania (JET), umemchangua Dk.Elen Utaro, kuwa mwenyekiti wake kwa
kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Dk.Utaro
ambaye alikuwa mgombe pekee katika nafasi hiyo, alipata kura za ndio
32 dhidi ya kura 13 zilizomkataa,wakati makamu mwenyekiti Ali Haji Hamad
wa Zanzibar alipata kura 41 za ndio na tatu zilimkataa.
Mkutano
huyo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa hotel ya Lion jijini
Dar-es-salaam na kusimamiwa vema na Mwanasheria Emmanuel Masawe,
uliwachangua wajumbe wa bodi na kura zao kwenye mabano kuwa ni Lea Moshi
(43), Andrew Chale (39), Judica Lasai (35), Bakari Kimwaga (34),na
Singi Mugumia (28). Jumla ya wajumbe 44 walipiga kura.
Awali
Makamu Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Aisha Dachi ambaye alisimamia
mkutano huo mkuu wa uchanguzi, alisema yeye binafsi hakutaka kutetea
nafasi yake hiyo,kwa madai kwamba hapendi mtindo wa ‘Ukurunzinza’.
Dachi
alisema ‘Ukurunzinza’ pamoja na madhara yake mengi, pia unabinya
demokrasia kwa vile unawanyima watu/wanachama wengine kupata nafasi ya
kuonyesha uwezo wa kutumikia chama chake.
“Ninyi
wenzetu tuliokuwa pamoja katika kipindi cha miaka mitatu
iliyopita,endelelezeni majadiliano mengi ambayo tumeyaanzisha na
tulikuwa hatujayapatia majawabu.Endelelezeni na simamieni kwa pamoja na
wenzenu wapya suala la kupata nyumba ua makazi ya chama chetu cha JET na
zaidi hakikisheni mnaongeza wanacha wengi zaidi kadri
mtakavyoweza”,alisema Dachi ambaye anaitumikia TBC taifa.
Awali
Katibu wa JET, Chrysostom Rweyemamu, alitaja baadhi ya shughuli kubwa
zinazotarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha mwaka wa 2015
kilichobakia,kuwa ni kusimamia utekelezaji wa miradi iliyopo na mabayo
haijaiva ya Ardhi Yetu Ajenda Yetu,mradi wa Mama Misitu na mafuta ya
gesi.
Alitaja
shughuli nyingine kuwa ni kuandaa ziara tano za waandishi wa habari
kutoka wilaya za Mufindi , Kilwa, Rufiji, Kilolo na Mbarali kwa ajili ya
kukusanya ushahidi na taarifa za mabadiloko hasi na chanya ya
utekelezaji wa mradi wa Ardhi Yetu Ajenda Yetu
TUKUTANE FACEBOOK KWA KUBOFYA HAPA>>>FB<<<




Leave a Comment