HII NDIO HUKUMU ILIYOTOLEWA NA BASATA KUHUSU SAKATA LA PICHA ZA UCHI ZA "SHILOLE"

Shilole a.k.a Shishi
bybee sasa anaweza kupata usingizi mnono bila mawazo, sababu lile sakata
la kusambaa kwa picha zake chafu zilizopigwa wakati akitumbuiza nchini
Ubelgiji mwezi uliopita hatimaye limemalizika vizuri.
Sakata hilo ambalo
lilifika hadi bungeni ambapo Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na
Michezo, Juma Nkamia alisema serikali ililiagiza Baraza la Sanaa la
Taifa, BASATA kufanya naye mahojiano ili serikali iweze kuchukua hatua.
Muimabji huyo wa ‘Nakomaa na Jiji’ ameelezea furaha yake baada ya kusamehewa na BASATA alipoenda kutoa maelezo.
“Leo nimeenda BASATA
kwasababu waliniita juzi, kwahiyo nimeenda kusikiliza wito wao,
tumeongea nashukuru wamenielewa tumeongea tumeelewana basi hakuna tena
ambacho kitu kina tatizo tena hapo kwasababu wale ni wazazi wanatakiwa
kumkanya mtu kama mtoto labda” Alisema Shishi bybee
“Tumeelezana pale nini
kifanyike nini kisifanyike na kila kitu ambacho kinahusiana na tasnia ya
sanaa. Nimewaelezea situation ilivyotokea wamenielewa wameniambia pia
niwe mwangalifu katika mavazi, of-course ni kweli kitu kama hicho
kinaweza kutokea kwahiyo sisi ni binadamu, nimeshukuru sana kwasababu
wameweza kunielewa, basi ni hivyo tu nina furaha kwaajili ya hiyo kitu.”
Alimaliza Shilole.
Source: EATV.TV
Leave a Comment