KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA ASISITIZA WANANCHI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI YA KUDUMU LA WAPIGA KURA.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt.
Rajab Rutengwe akiwa ameshika mwenge wa Uhuru baada ya kupokea kwa Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Mhe. Said Magalula
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt.
Rajab Rutengwe (kushoto) akiwa amekumbatiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Mhe. Said Magalula baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa
uhuru kitaifa Bw. Juma Khatibu Chum akifungua kitambaa kama ishara ya
kuzindua zoezi la uandikishaji wapiga kura Wilayani Mvomero
lililofanyika katika Kijiji cha Salawe Kata ya Kibati.
Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa
Bw. Juma Khatib (katikati) akipewa maelezo ya zoezi la uandikishaji wa
wapiga kura litakavyoendeshwa, muda mfupi baada ya kuzindua zoezi hilo.
(Kulia mwenye tracksuit) ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Betty Mkwasa.
……………………………………………………………………..
Na. Andrew Chimesela -Morogoro
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa
uhuru Kitaifa Ndugu juma Khatibu Chum amewataka wananchi wa Mkoa wa
Morogoro kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili kutumia haki
yao ya msingi ya kuchagua viongozi kwenye uchaguzi Mkuu utakaofanyika
mwezi Oktoba mwaka huu.
Juma Kghatibu ameyasema hayo leo wakati akitoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa mkesha wa mwenge eneo la Kichangani katika Tarafa ya Tuliani Wilayani MvomeroMkoani Morogoro.
Amesema mwananchi yeyote ambaye amefikisha umri wa mika 18 na mwenye sifa zote za kuandikishwa aende kujiandikisha ili aweze kupata fursa ya kuchagua viongozi bora watakaoiongozi nchi katika Serikali ya awamu ya tano.
“Hakuna nchi yeyote duniani yenye maendeleo bila ya viongozi bora. Na huwezi kupata viongozi bora nje ya uchaguzi Mkuu. Ni lazima tujiandikisha na kuchagua viongozi bora itakapofika mwezi Oktoba, uchaguzi ni haki yetu ya kidemokrasia, na ni haki yetu ya Kikatiba”. alisema Bwana Khatibu.
Mapema akiwa Wilayani Mvomero ikiwa ni Wilaya ya kwanza kukimbiza mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Morogoro, Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge Kitaifa alizindua zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa kutumia mfumo wa BVR katika kijiji cha Salawe kilichoko Kata ya Kibati Wilayani humo tayari kwa zoezi hilo kuanza hapo Juni, 16, 2015.
Aidha, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, alikemea suala la rushwa akiwataka wananchi kuacha kupokea rushwa kwa kuwa inasababisha kuwapata viongozi wabovu.
Pia, alisisitiza kutumia vyandarua kadri ya malengo ya serikali ili kupambana na malaria badala ya kutumia vyandarua hivyo kwa malengo tofauti.
Kuhusuna ugonjwa hatari wa Ukimwi, alisema waliokwisha ambukizwa ugonjwa huo ni vema kuanza kutumia dawa za ARV na kula vyakura bora mapema na kufuata ushauri unaotolewa na madaktari.
Awali akipokea Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Rajabu Rutengwe alibainisha kuwa jumla ya miradi 51 itapitiwa na mwenge wa uhuru katika Mkoa wa Morogoro. “Mwenge wa Uhuru ukiwa ndani ya Mkoa wa Morogoro utakimbizwa ndani ya Wilaya 6 ukipitia jumla ya miradi 51 yenye thamani ya shilingi 9,750,540,533.40” Alisema.
Aliongeza kuwa “kati ya hizo, michango ya wananchi ni shilingi,2,522,160,236.00, Halmashauri 574,640,680.00, Serikali Kuu 4,734,382,176.40.00 na wafadhili 1,919,357,441.00.
Mwenge wa Uhuru, kesho utaanza mbio zake Wilaya ya Gairo ambapo utapitia jumla ya miradi sita.

Nipate facebook kwa kubofya hapa>>>FB<<<

Leave a Comment