MUFTI Mkuu wa Tanzania, Sheikh Issa Bin Shaaban Simba, afarikki dunia
Mufti
Mkuu wa Tanzania, Sheikh Issa Bin Shaaban Simba, amefariki dunia
alfajiri ya leo katika hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam.
Taarifa
kutoka mamlaka husika na dini na ndugu wa karibu walieleza kuwa, mwili
wa marehemu umeondolewa hospitali hapo na kuhamishiwa hospitali kuu ya
Jeshi ya Lugalo kungoja taratibu za mazishi.
Kwamujibu
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema kuwa
marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo pamoja na presha. Mwili
wa marehemu utasafirishwa kesho mkoani Shinyanga kwaajili ya maziko.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un
إِنَّا للهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ)
Kwa
upande wake, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa
Dkt. Fenella Mukangara (Mb.) ametuma salamu za rambirambi kwa Baraza
Kuu la Waislamu Nchini (BAKWATA) na Waislamu wote nchini kufuatia kifo
cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba kilichotokea
Jumatatu, tarehe Juni 15,2015 katika hospitali ya TMJ Jijini Dar es
Salaam alipokuwa anatibiwa.
Katika
salamu hizo, Mhe. Mukangara amesema kuwa ni jambo la kusikitisha
kumpoteza kiongozi huyo ambaye bado Taifa lilikuwa likimuhitaji hasa
katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka
huu.
Waziri
huyo ameongeza kuwa Mufti atakumbukwa kwa upole , unyenyekevu wake na
kutopenda makuu,wakati wa uhai wake marehemu alikuwa tayari kumsikiliza
kila mtu bila kujali dini au kabila lake.
“Nimepokea
kwa huzuni nyingi taarifa ya kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti
Shaaban Issa Bin Simba ambaye alikuwa Kiongozi anayeshirikiana vizuri na
viongozi wote wa serikali na vyama mbalimbali katika kuhakikisha
Watanzania wanaendelea kuwa wamoja” amesema .
Amesema
Waziri Mukangara: “Nakutumia salamu zangu za rambirambi wewe Katibu
Mkuu, BAKWATA na waislamu wote nchini na naungana nanyi katika
kuomboleza msiba huu mkubwa katika nchi yetu.
Aidha,
kupitia BAKWATA, natuma salamu za dhati ya moyo wangu kwa familia ya
marehemu kwa kumpoteza mpendwa wao. Napenda wajue kuwa msiba wao ni
msiba wangu. Pia, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa
Rehema aiweke pema peponi roho ya marehemu … Amina.”
Imetolewa na; Idara ya Habari(MAELEZO)

Leave a Comment