Mtambo wa kuzalisha Bunduki za kienyeji wakamatwa
Watuhumiwa 19 wamekamatwa mkoani Rukwa na mtambo wa mtambo wa kutengeneza bunduki za kienyeji pamoja na silaha za aina mbalimbali zikiwemo bunduki 30 na risasi 231.
Silaha hizo zimekamatwa kufutia msako uliofanywa na Polisi ambapo mbali na silaha hizo waliweza pia kukamata meno na mikia miwili ya tembo.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema jana mjini kuwa silaha hizo zilikamatwa kutokana na operesheni ya kupambana na visa vya ujangili na uhalifu mwingine katika maeneo mbalimbali ndani ya mkoa huo.
Ameongeza kuwa silaha hizo zilizokamatwa zinasadikiwa kutumika katika matukio ya kijangili na uhalifu mwingine ambapo baadhi ya bunduki zimegundulika kuwa zinamilikiwa kihalali.
Kwa upande wa silaha zilizokamatwa ametaja kuwa ni bunduki aina ya shotgun 8, rifle 8, magobori 4, bunduki 6 aina ya shotgun zilizotengenezwa kienyeji, risasi 5 za SMG, risasi 53 za rifle na risasi 173 za shotgun.
Watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote baada ya uchunguzi wa awali wa kukamilika.

Leave a Comment