PIGO LINGINE!! BANZA STONE AFARIKI DUNIA MCHANA HUU


Mwanamuziki nyota wa muziki wa dansi, Ramadhani Masanja 'Banza Stone', amefariki dunia.


Banza amefariki dunia alipokuwa amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Mwanamuziki huyo nyota wa zamani wa Twanga Pepeta na Tot alikuwa amelazwa hospitalini muda mrefu.

Mmiliki wa Twanga Pepeta, Asha Baraka amethibitisha kifo cha Banza Stone.

“Kweli amefariki leo saa saba, baada ya kutoka tu msikitini ndiyo tumepata taarifa hizo za msiba,” alisema Asha Baraka.


Mara kadhaa, Banza amekuwa akizushiwa kifo kupitia mitandao na vyombo mbalimbali vya habari.
KWA MSAADA WA MTANDAO WA  SALEHJEMBE

No comments

Theme images by sbayram. Powered by Blogger.