WAZIRI MKUU KUANZA ZIARA MKOANI RUVUMA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Ruvuma, ambapo
atawasili mkoani hapo leo saa tisa alasiri.
Baada ya Waziri Mkuu kuwasili
Uwanja wa Ndege wa Songea, atapokelewa na viongozi wa Chama na Serikali,
pia atakwenda Ikulu kupokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Ruvuma.
Aidha, siku ya jumatatu atakuwa
na shughuli za kufungua tawi la Benki ya Posta mjini Songea, kukagua
maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) kanda ya Songea
na kukagua makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Siku inafuata atatembelea na kukagua Hospitali ya Rufaa ya mkoa, na baadaye kuzungumza na watumishi wa hospitali hiyo.
Siku ya nne ya ziara yaani
jumatano, Waziri Mkuu atafanya majumuisho ya ziara mkoani humo, kabla ya
kuagana na viongozi wa Chama na Serikali na kurejea Dar es Salaam.
Leave a Comment