HII NDIO KATIBA YA MAPENZI.... NAOMBA KUWASILISHA!
Unajua
katiba? Ni muundo wa sheria, kanuni zinazoainisha jinsi ambavyo nchi, chama au
shirika vitakavyoendesha shughuli zao.
Uhusiano wa kimapenzi upo katika mtindo wa kitaasisi lakini kwa
bahati mbaya katiba yake haipo kwenye maandishi (non-written constitution).
Makala haya yataiweka katiba hiyo kwenye maandishi kwa ajili ya kukusaidia msomaji wangu kujua jinsi ya kuishi ndani ya uhusiano wako.
Uhusiano wa kimapenzi upo katika mtindo wa kitaasisi lakini kwa
bahati mbaya katiba yake haipo kwenye maandishi (non-written constitution).
Makala haya yataiweka katiba hiyo kwenye maandishi kwa ajili ya kukusaidia msomaji wangu kujua jinsi ya kuishi ndani ya uhusiano wako.
Wengi
wamekuwa wakipata tabu, wanapotoka na kuishi nje ya mistari inayofaa kwa
sababu hawajaisoma au hawaijui.
Unahitaji
muongozo wa kikatiba ili mapenzi yako yasitawaliwe na migogoro. Unatakiwa ujue
jinsi ya kuishi kwa upendo na furaha.
Amani
itawale kwenye uhusiano, hali kadhalika tabia zako zikidhi
mahitaji
ya katiba ya mapenzi au ndoa yako.
Je,
unatakiwa uyafanyie nini mapenzi yako au ndoa yako? Muonekano wako uweje mbele
ya mwenzi wako?
Ukiwa
na hasira, ni kitu gani cha kufanya? Inapotokea mpenzi wako ameghadhabika, jambo
lipi ufanye liweze kumrudisha kwenye mstari unaotakiwa?
Ndoa
inahitaji nini? Kwa nini aliye kwenye ndoa hatakiwi kujiona ana uhuru wa
kupitiliza kiasi cha kumuathiri mwenzi wake? Nini wajibu na haki za mtu
kwenye mapenzi? Ni kwa namna gani mtindo wa
maisha
wa bachela, ukitekelezwa na mwanandoa ni sumu?
Hayo
na mengine mengi, yanachambuliwa kinagaubaga kwenye katiba ya mapenzi.
Mtu
sahihi ni yule anayeishi kwa kujiamini, si ambaye anafanya kwa kujaribu,
akisubiria matokeo au mapokeo ya mpenzi
wake.
Mapenzi
ni rahisi mno endapo utaheshimu muongozo.
Katiba
yenyewe inaundwa na vipengele vingi ambavyo nitavichambua katika wigo mpana ili
uweze kuelewa ipasavyo.
Inahitaji
utulivu na umakini wakati wa kusoma, mwisho utakuwa ni mwenye
mafanikio
makubwa endapo yaliyomo kwenye maandishi yangu yatakita vilivyo ndani ya
ubongo.
UPENDO
Hiki
ni kipengele kikuu.
Unaweza
kukiita kifungu mama ndani ya katiba ya mapenzi. Huwezi kusema
upo
kwenye uhusiano makini kama upendo haupo katikati. Chukua hatua madhubuti
endapo utabaini upendo haupo.
Mkatae
mwenzi ambaye hakupendi, kinyume chake atakupa mateso mbele ya safari.
Muongozo
wa kipengele cha upendo ni kwamba lazima wewe mwenyewe uanze kuwekeza upendo
kisha naye akupende.
Ni
maisha ya ubinafsi kutaraji kupendwa, wakati wewe mwenyewe huoneshi kwa
mwenzako. Zingatia hili kila siku na wakati wote ili uweze kufaidi matunda
mema kwenye uhusiano wako.
Kuna
tabaka la watu ambao huishi kwa kusikilizia zaidi.
Haitakiwi
kutegea, upendo unamaanisha pande mbili zinazovutana.
Huyu
anatekeleza hili kwa ajili ya mwenzake, hali kadhalika na mwingine
anasimama imara kuhakikisha mpenzi wake anafaidi malisho mema
ya
mapenzi.
Hakikisha
mpenzi wako hakushindi upendo, onesha unampenda zaidi.
Upendo
huyeyusha mengi. Ukiwekeza upendo kwa mwenzi wako, utamfanya nafsi yake iwe na
woga.
Ni rahisi
kushinda vishawishi, kama atakuwa akikaa peke yake anakuwa anajiridhisha kuwa
unampenda kwa
moyo
wako wote.
Vinginevyo,
anaweza kushawishika na kukusaliti kama tu akili yake itamtuma kuamini kwamba
humpendi.
Hivyo
basi, hakikisha upendo wako si wa wasiwasi. Mfanye awe na imani, ikibidi imani
ya kupitiliza.
Utafiti
unaonesha kuwa mtu aliyeonesha upendo mkubwa kisha akasaliti kwa tamaa
zake, anapobainika na kuachwa hujuta zaidi kuliko yule aliyeona hakukuwa
na upendo kwa sababu haoni cha kupoteza.
Chukua
hatua madhubuti endapo utabaini upendo haupo. Mkatae mwenzi ambaye hakupendi,
kinyume chake atakupa mateso mbele ya safari.
Kuna
faida kubwa mbele ya safari endapo utamkataa asiyekupenda au usiyempenda
leo, kuliko kumng’ang’ania, kwani itakutesa.
Muongozo
wa kipengele cha upendo ni kwamba lazima wewe mwenyewe uanze kuwekeza kisha
naye akupende.
Ni
maisha ya ubinafsi kutaraji kupendwa wakati wewe huoneshi kwa mwenzako.
Zingatia
hili kila siku na wakati wote ili uweze kufaidi matunda mema kwenye
uhusiano wako.
Kuna
tabaka la watu ambao huishi kwa kusikilizia zaidi. Haitakiwi kutegea, upendo
unamaanisha pande mbili zinazovutana.
Huyu
anatekeleza hili kwa ajili ya mwenzake, hali kadhalika na mwingine anasimama
imara kuhakikisha mpenzi wake anafaidi malisho mema ya huba.
Hakikisha
mpenzi wako hakushindi upendo, onesha unampenda zaidi.
Upendo
huyeyusha mengi. Ukiwekeza upendo kwa mwenzi wako, utamfanya nafsi yake iwe na
woga.
Ni
rahisi kushinda vishawishi, kama atakuwa akikaa peke yake atakuwa akijiridhisha
kuwa unampenda kwa moyo wako wote.
Vinginevyo,
anaweza kushawishika na kukusaliti kama tu akili yake itamtuma kuamini humpendi.
Hivyo
basi, ...hakikisha upendo wako si wa wasiwasi. Mfanye awe na imani, ikibidi iwe
ya kupitiliza.
Utafiti
unaonesha kuwa mtu aliyeonesha upendo mkubwa kisha akasaliti kwa tamaa zake,
anapobainika na kuachwa hujuta zaidi kuliko yule aliyeona hakukuwa na
upendo kwa sababu haoni cha kupoteza.
1.HOFU
Wengi
hawajui hili. Unaweza kuwa na upendo mkubwa kwa mwenzi wako lakini kama huna
hofu juu yake ni sawa na bure.
Katika
kipengele hiki, nashauri watu kujitenga na maneno yasiyo na faida.
Mapenzi
siyo tamko la kinywa peke yake, moyoni ndimo mahali pake.
Hii
inamaanisha kuwa mapenzi hayatamkwi midomoni na yakaisha. Ni lazima mwili mzima
uhusike kivitendo.
Mantiki
hapo ni kuwa unaweza kusema unapenda lakini kama huna hofu yoyote kwa
huyo umpendaye ni sawa na kupiga gitaa kumtumbuiza mbuzi, kwani hakutakuwa
na matokeo mazuri.
Faida
ya hofu kwenye uhusiano ni kuwa kila nukta, dakika, saa na siku, utaishi kwa
tahadhari. Lile ambalo unajua haliwezi kumpendeza mwenzi wako,
hutalitenda, hivyo kufanya maelewano kuwa makubwa
zaidi.
Husaidia
kuepusha migogoro na kuumizana bila sababu za msingi.
Kiburi
kimejikita kwenye vichwa vya watu wengi, hivyo kufanya hata yale ambayo wapenzi
wao hawataki.
Mathalan,
mtu anaweza kutambua kuwa akivaa nguo za aina fulani, mpenzi wake hawezi kufurahi
lakini kwa sababu ya kutokuwa na hofu, anavaa na kuibua ugomvi usio wa lazima.
Mtu
anajua kwamba mwenzi wake hapendelei tabia ya kutembea usiku lakini kwa sababu
ya kiburi, anasaga rumba mpaka usiku wa manane ndiyo anarudi nyumbani. Ni
kutafuta shari, hiyo ni tabia ya
kutopenda
amani na mwenzi wako.
Sisemi
uogope ila unatakiwa uwe na hofu kutoka moyoni.
Kila
jambo linalotokea, hebu jiulize mara mbili mpaka tatu. Ukiona ni zito, jipe
muda zaidi wa kutafakari kabla hujaamua.
Inawezekana
ukalichukulia ni dogo, kumbe mwenzako akalitafsiri kwa
undani
zaidi, mwisho akaona muachane kwa sababu amehisi unamdharau. Zingatia kwamba
kufanya jambo la kumkera mpenzi wako kwa makusudi ni dharau.
Mimi
kama mchambuzi wa masuala ya mapenzi, nimegundua baada ya utafiti wangu kuwa
asilimia kubwa ya migogoro kwenye mapenzi hutokea kwa sababu ya wawili
wanaoamua kupendana kukosa hofu.
Hoja
hapa ni kwamba ukiishi kwa kujiamini kupita kiasi mbele ya mwenzi wako ni
janga. Ni sawa na kuuweka uhusiano wenu hewani.
Sina
maana kuwa watu wasijiamini, mantiki ni kwamba kila mmoja ajipe hofu kwenye
matendo yake ili asimkere mwenzake.
Ajue
kuwa dogo linaweza kuhatarisha mapenzi, kwa hiyo hatakiwi kuthubutu kutenda.
Uhusiano wa kimapenzi huunganisha pande mbili zenye matarajio ya furaha, kwa
hiyo ni vizuri kuishi kwa kuheshimu matarajio hayo.
Lile
ambalo unajua haliwezi kumpendeza mwenzi wako, hutalifanya, hivyo kufanya
maelewano kuwa makubwa zaidi.
Husaidia
kuepusha migogoro na kuumizana bila sababu za msingi.
Kiburi
kimejikita kwenye vichwa vya watu wengi, hivyo kufanya hata yale ambayo wapenzi
wao hawataki.
Mathalan,
mtu anaweza kutambua kuwa nikivaa nguo za aina fulani, mpenzi wake hawezi
kufurahi lakini kwa sababu ya kutokuwa na hofu, anavaa na kuibua ugomvi
usio wa lazima.
Mtu
anajua fika kwamba mwenzi wake hapendelei tabia ya kutembea usiku lakini kwa
sababu ya kiburi, unasaga rumba mpaka usiku wa manane ndiyo unarudi
nyumbani.
Ni
kutafuta shari, hiyo ni tabia ya kutopenda amani na mwenzi wako.
Sisemi
uogope, ila unatakiwa uwe na hofu kutoka moyoni.
Kila
jambo linalotokea, hebu jiulize mara mbili mpaka tatu. Ukiona ni zito, jipe
muda zaidi wa kutafakari kabla hujapata uamuzi sahihi.
Inawezekana
ukalichulia ni dogo, kumbe mwenzako akalitafsiri kwa undani zaidi, mwisho
akaona muachane kwa sababu amehisi unamdharau.
Zingatia
kwamba kufanya jambo la kumkera mpenzi wako kwa makusudi ni dharau.
Kama
mchambuzi wa masuala ya mapenzi, nimegundua baada ya utafiti wake kuwa asilimia
kubwa ya migogoro kwenye mapenzi hutokea kwa sababu ya wawili wanaoamua
kupendana kukosa hofu.
Hoja
hapa ni kwamba ukiishi kwa kujiamini kupita kiasi mbele ya mwenzi wako ni
janga. Ni sawa na kuuweka uhusiano wenu hewani.
Sina
maana kuwa watu wasijiamini, mantiki ni kwamba kila mmoja ajipe hofu kwenye
matendo yake ili asimkere mwenzake.
Ajue
kuwa dogo linaweza kuhatarisha mapenzi, kwa hiyo hatakiwi kuthubutu kutenda.
Uhusiano wa kimapenzi, huunganisha pande mbili zenye matarajio ya furaha, kwa
hiyo ni vizuri kuishi kwa kuheshimu matarajio hayo.
UAMINIFU
Kifungu
hiki kina vifungu vidogo viwili.
Mosi: Uaminifu binafsi. Yaani mhusika
anakuwa anasukumwa kutorahisi mwili wake kutumika kiholela kutokana na kulinda
heshima yake.
Hii
ina maana ya nidhamu binafsi. Nitoe msisitizo kwamba mwenzi bora wa maisha ni
yule anayejitunza kwa nidhamu binafsi. Nidhamu ya woga inasaidia lakini si
nzuri sana.
Pili: Ni uaminifu unaotokana na hofu.
Mtu
anakutana na vishawishi vya hapa na pale lakini anaogopa kuingia kwenye
uhusiano wa pili kwa sababu ya hofu aliyonayo kutokana na macho ya jamii
inayomzunguka.
Anajua
watu wakijua watamuona mhuni (malaya), anataka aheshimike, kwa hiyo anabaki na
uaminifu wake wa woga.
Katika
kipengele hicho cha woga, anaweza pia kuogopa kusaliti kwa sababu anajua za
mwizi ni arobaini. Anatambua kwamba ipo siku mwenzi wake atajua na kuanzia hapo
penzi ..litakufa.
Naye
hataki uhusiano wake ufe, kwa hiyo anajilinda, ingawa ndani yake kunakuwa na
msukumo wa kuanzisha figa la pili na tatu. Hata huu nao ni uaminifu.
Ogopa
mno mwenzi ambaye haoni cha kupoteza.
Huyo
anaweza kukufanyia jambo baya wakati wowote.
Anaweza
kuanzisha uhusiano mwingine katika kipindi ambacho bado unamhitaji.
Anaweza
kukuacha na asijali maumivu yako. Hivyo basi, tazama uendako, mtathmini mwenzio
kama ana sifa zinazofaa kisha
amua
kwa faida yako mwenyewe.
HESHIMA Unahitaji mpenzi
ambaye anajiheshimu. Weka akilini hilo halafu lifanye kuwa muongozo wa maisha
yako ya kimapenzi. Heshima ina matawi mengi lakini muhimu kwako ni kuwa lazima
awe anakidhi vipengele vyote.
Wengi
wanateswa na mapenzi leo hii kwa sababu hawakuzingatia kipengele cha heshima
wakati wanaamua kuhusu hatma ya uhusiano wao.
Lazima
awe anajiheshimu.
Nalilisisitiza
hilo kwa mara ya pili kwa sababu kama hana heshima binafsi,maana yake hatakuwa
nayo ya kumpa mwingine.
Watu
wanaojiheshimu ndiyo haohao huwaheshimu wengine.
Nakuomba
ulizingatie hilo kwa umakini mkubwa kwa sababu huamua furaha ya wapenzi,
wachumba na hata wanandoa.
Mtu
asiyejiheshimu anaweza kufanya jambo lolote na wakati wowote.
Anaweza
pia kutoheshimu umuhimu wa mwenzi wake.
Tia
akilini kuwa mtu asiyejiheshimu huwa hana soni mbele ya macho ya jamii. Anaweza
kugombana na watu sehemu yoyote hata ukweni kwake.
Anaweza
kuvaa nguo za ‘kishenzi’ ambazo zitamuacha kwenye aibu mwenzi wake. Yeye hawezi
kuona aibu, kwani hajiheshimu. Binadamu wengi hujipa mizigo mibaya kwa kuzoa
watu ambao hawajui kujistahi, mwisho wanapata tabu kuwarekebisha.
Wanasema,
samaki mkunje angali mbichi, sasa wazazi na familia yake, walishindwa
kumuweka sawa, wewe utawezaje wakati
ameshakubuhu?
Tia
akilini.
Leave a Comment